Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtori ndizi zinasagwa/kupondwa, hapo hakuna maelekezo ya mtori...Hii ni mtori au ndovi?
Mahitaji
- Ndizi Mbivu: 6
- Nazi: Kikopo 1
- Sukari: Vijiko 3 vya chakula
- Hiliki: Kijiko 1
Namna ya Kutayarisha/Kupika
- Menya ndizi kisha zipasue kati utoe ule moyo wa kati.
- Zikate size unayopenda mwenyewe, kisha uzipange ndani ya sufuria.
- Weka maji kiasi na uzichemshe ndizi kidogo, karibu ya kuiva mimina tui.
- Mimina sukari na hiliki ndani ya ndizi na ziwache zichemke mpaka tui libaki kidogo.
- Ziondoe jikoni na uziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa

Nice and simple, asante @ chief cook.
Kuna ndizi zinaitwa bokoboko, zikiiva zinatengenezwa banana fritters.
1. Osha ndizi zilizoiva kiasi, kisha menya na kupasua katikati
2. Chekecha unga kwenye bakuli kiasi. Tia chumvi a pinch
3. Pasua yai moja ama mawili ndani ya unga. Anza kukoroga na mwiko wa mbao ama plastic ama spatula kwa mizunguko ya duara upande mmoja tu. Ni kama unakoroga chapati za kumimina. Mchanganyiko uwe na uzito wa uji unaomiminika taratibu.
4. Weka mafuta kiasi kwenye kikaango ama frier. Pasha moto
5. Tumbukiza ndizi bokoboko zilizomenywa ndani ya mkorogo wa unga, chomoa na uma na uweke kwenye mafuta ya moto kiasi. Geuza pande zote ziwe brown.
6. Ipua kwa kutumia uma ili kuchuja mafuta, weka kwenye chujio ama sahani yenye bloating ama kitchen paper.
Zinafaa kama snack ama mlo zikiambatana na mboga za majani na kitoweo. Zinafaa kwa safari, take away ama picknick.
Hapa mimi mimate tu duuuu natamanije.

Naomba kuwakilisha.