Nawezaje kuwa na furaha na amani ya roho?

Nawezaje kuwa na furaha na amani ya roho?

Nimekuwa myonge na nafsi Yangu inasononeko.

Sikosi chakula wala pakulala...Ila nakosa furaha moyoni, naona uzito rohoni mwangu, nakosa furaha kabisa.

Naona mambo yangu nashindwa yabeba.

Najitahidi kusali na kukumbuka maandiko ya Mungu, napata afueni kwa muda.

Japo najipa moyo kuwa kwenye uzito Kuna wepesi...Naamini nothing last forever not even our troubles.

Kuna muda nikitembea barabarani nikiona watu wanacheka nahisi wananicheka Mimi.

Huu Uzi hauhusu mahusiano ya kimapenzi kabisa.

Sinywi pombe, sivuti Bangi wala sigara.

Nifanyaje kupunguza Hali ya sononeko moyoni mwangu.
Nini sababu ya hiyo sononi yako,maana umeshatugusia kwamba haihusiani na mapenzi,tujuze tujue wapi tunaanza kukushauru
 
Nini sababu ya hiyo sononi yako,maana umeshatugusia kwamba haihusiani na mapenzi,tujuze tujue wapi tunaanza kukushauru
Mkuuu...wakati naweka hili bandiko nilikua naumwa....

Ila kwa uwezo wa Allah...nimepona
 
Acha kutumia muda mwingi pekee yako kama kujificha kwenye mitandao ya kijamii huku ukidhani umejichanganya na watu.

Pia usipende kujilinganisha maisha yako na mwingine. Mfano sababu mtu fulani alipata mume kwenye umri fulani basi na wewe unahisi mambo yatakuwa hivyo hivyo.

Weka malengo yako mwenyewe kupitia hayo pambana kufanikisha bila kuangalia watu wengine.

Take it easy kwanini ukose amani wakati tunaishi mara moja.

Kuna watu wanatamani hali uliyonayo furahia na shukuru ulichonacho maana wengine wanakitafuta ila hadi leo hawajapata.
Fact
 
Back
Top Bottom