Nawezaje kuwa na hati miliki

Nawezaje kuwa na hati miliki

msani

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Posts
1,801
Reaction score
1,191
Habari wana JF:
Kwanza nawashukuru sana kwa kujitoa kwenu kwa matatizo ya wengine.Heshima kwenu ndugu zangu.

Pili,nilikuwa na wazo la mradi fulani kipindi cha takribani miaka miwili bahati mbaya au kutoelewa kwangu nilipoteza mradi huo kwa kushirikisha watu ambao walinizidi uwezo na kuuchukua kama wao na kwakuwa ulikuwa wa mtaji mkubwa sana nikashindwa.
Lakini hivi sasa nina project nyingine ambayo nimeishakusanya taarifa zoote za soko na utekelezaji wake nimeona unafaa na unafaida kubwa ila mtaji wake ni mkubwa sana.
Sasa naogopa jinsi ya kuwashirikisha watu kwa kukumbuka lililonikuta kwenye project ya kwanza.
Je,nawezaje kumiliki wazo hili ili hata kama nikiamua kumshirikisha mtu asiwe na uwezo wa kufanya bila ruhusa yangu mimi,yaani niwe na nguvu kisheria.
naombeni ushauri maana kuna muwekezaji mmoja ameomba nimpe full details nimegoma kwanza
 
Back
Top Bottom