Mkuu kwema?
Unatakiwa uwe na leseni ya biashara yenye zaidi ya miaka 2 (Kwa NMB) au miezi 18 kwa CRDB, Leseni iwe ya biashara nyingine, yani isiwe unataka kuitegemea hiyo kama biashara pekee.
Biashara iwepo kwenye fremu yenye usalama, watakuja kuipiga picha frem yenyewe.
Kwa CRDB utatakiwa ulipe TZS 236,000/= kama sijakosea, kwa ajili ya mashine na zile karatasi zao, hawakulazimishi uweke kiasi flan cha float kwa kuanzia.
Kwa NMB wanataka laki2 kwa ajili ya mashine na vifaa vingine, ila wanakulazimisha uweke float ya walau milion 2 kwa kuanzia (hii unaweka kila kitu kiko tayar, na hii pesa ndo mtaji wako).
Ili uanze huduma hii unatembelea ofisi iliyokaribu yako tu watakupa mwongozo uanze vipi