Nawezaje kuwa Wakala wa benki. Mfano NMB na CRDB

asante sana mkuu, mi pia nipo dar, ntamcheki
 
vigezo na sifa ili mtu kupewa uwakala wa bank hapa tanzania na vp mchnganua wa hii biashara uko vp yaan faida pia mtaji ni kiasi gani
 
fahari huduma inafaida kuliko hata tigo pesa uwakala wake unapatika tawini mimi ni mmoja wa mawakala
Una huduma uwakala wa NMB manake niliomba uwakalawakanipa masharti ya nikatimiza yote wakaniambia niko tayari nimeruhusiwa niliweka kias cha mil 2 laki 2 ili wanipe mashine nina wik ya pili sasa sijapata mashine wewe ilikuaje mkuu?
 
Evolrm naomba makato ya kutoa pesa kwa wakala wa Fahari Huduma
Nataka kutoa zaidi ya laki tano
 
nielekeze mkuu ulianzia wapi nami nahitaji kuwa wakala mkuu
Una huduma uwakala wa NMB manake niliomba uwakalawakanipa masharti ya nikatimiza yote wakaniambia niko tayari nimeruhusiwa niliweka kias cha mil 2 laki 2 ili wanipe mashine nina wik ya pili sasa sijapata mashine wewe ilikuaje mkuu?
 
jamani mnaojua njooni mtujaze maarifa
 
jamani mnaojua njooni mtujaze maarifa
Mkuu kwema?

Unatakiwa uwe na leseni ya biashara yenye zaidi ya miaka 2 (Kwa NMB) au miezi 18 kwa CRDB, Leseni iwe ya biashara nyingine, yani isiwe unataka kuitegemea hiyo kama biashara pekee.

Biashara iwepo kwenye fremu yenye usalama, watakuja kuipiga picha frem yenyewe.

Kwa CRDB utatakiwa ulipe TZS 236,000/= kama sijakosea, kwa ajili ya mashine na zile karatasi zao, hawakulazimishi uweke kiasi flan cha float kwa kuanzia.

Kwa NMB wanataka laki2 kwa ajili ya mashine na vifaa vingine, ila wanakulazimisha uweke float ya walau milion 2 kwa kuanzia (hii unaweka kila kitu kiko tayar, na hii pesa ndo mtaji wako).

Ili uanze huduma hii unatembelea ofisi iliyokaribu yako tu watakupa mwongozo uanze vipi
 
shukran mkuu nimepata mwanga sasa duuuh hapo kweny lessen iliyotimiza hiyo miaka ndo kimbembe my dear
 
shukran mkuu nimepata mwanga sasa duuuh hapo kweny lessen iliyotimiza hiyo miaka ndo kimbembe my dear
hata mimi nafuatilia hiyo, na leseni haikukamilisha huo muda. sasa nimefoji copy ya leseni ya zamani afu nikawapa na ya mwaka huu.

nimeshasubmit request yangu. so usiponiona hapa jukwaani ujue nimekamatwa kwa kufoji nyara za serikali [emoji23] [emoji23]
 
naomba uzidi kunifafanulia wanachukua muda gami hadi kukamilishiwa zoezi lako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…