Nay Wa Mitego ajifilisi, sasa arudi kutembelea bajaji

Nay Wa Mitego ajifilisi, sasa arudi kutembelea bajaji

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Kumekuwa na taarifa mbalimbali zikiendelea kusambaa juu ya Nay Wa Mitego kufulia mpaka kufikia hatua ya kuuza magari yake yote na sasa ameonekana mara kadhaa akitembea na bajaji hali ambayo haikuwa kawaida yake.
Bajaji+pic.jpg


Akizungumza hilo Nay Wa Mitego alisema ni kweli ameamua kuuza magari yake yote ila kwa sababu anazojua yeye na si kama watu wengi wanavyosema.

“Kila mtu anazungumza lake ujue, lakini kama kuuza nimeuza kwa sababu zangu za msingi, nimemua kuachana na magari nipande daladala na bajaji, na hayo ndio maisha ambayo nimekulia, unajua mimi nimezaliwa kwenye maisha ya kawaida na mtaa ndio umenilea, kwa hiyo watu
wasichoke kunipa lifti wakiniona, au wasishangae siku wakiniona natembea kwa mguu,” alisema


Chanzo: Mwanaspoti
 
Si huyu huyu alisema mungu wake kila akimwomba chochote anampa?? Aliimba wimbo fulani hapa kati akadokeza na kwamba anataka kugungua kanisa ili afanyie biashara! Au ndo ameanza kuwekeza kwenye huo ujenzi?? Any way mungu wake ndo anamjua!
 
Amekiuka maagano na miungu yake... miungu yake imeamua kumgeuka...

Kamwe usicheze na Mungu aliyeumba vyote,Mungu aliye hai... Mungu anayeweza yote.. MUNGUaliyekamata pumzi ya mwanadamu...
 
Back
Top Bottom