NaY wa mitego yuko sahihi au anakosea?

NaY wa mitego yuko sahihi au anakosea?

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
wasafitv-post-2021_05_05_17_34.jpg
Ametangaza kuanzia kesho anajitoa Basata kutokana na sheria zao kandamizi,hatopeleka tena nyimbo redioni bali atafanya mziki mtaani.
maamuzi ya Nay yamekuja baada ya wimbo wake wa Mama kupigwa pini na Basata.

Ikumbukwe tu Sheria ya Basata inataka msanii kabla ya kuachia wimbo wake apeleke Basata ili uhakikiwe ndipo upewe go ahead ama upigwe ban.

My take Basata kuna ukoloni flan hivi na mambo ya kishamba huenda kua waliopo kwenye hiyo ofisi ni aidha walokole,hawajui mziki wala hawana interest na wala hawafatilii mambo ya mziki,hawajui hastling za kitaa au ni washamba na malimbukeni ndio maana wanakurupuka kurupuka kwenye maamuzi yao.
 
Sheria zifuatwe maana maadili yamepotea na chanzo kikubwa ni mziki wa kizazi kipya.

Ney anajidanganya. Mkono wa sheria haukimbiwi. Ni sawa na mtu aseme anajitoa kuwa sio Mtanzania hivyo atakuwa anaua tu watu bila sheria kuchukua mkondo wake maana alishajitoa uraia.

BASATA itamfuata huko huko anakokimbia.
 
wewe Ney fata sheria wacha kutafuta huruma humu mitandaoni

Sent using Jamii Forums mobile app
No, Kama kweli nisheria basi ni kandamizi. Nay anatumia uhuru wa kutoa mawazo kwa mujibu wa katiba. Hajamtukana mtu, na ameuliza/ amesema mambo ambayo yapo mtaani. Hatuyasikii toka kwa watawala. Hata bungeni yakiongelewa yanapingwa kwa nguvu zote za dola. Mnataka hayo yasisemwe ni kwa manufaa ya nani? Acheni hizo, fikra hizo ziende na mwendazake.
 
Hivi basata uwa inawasaidiaje wasanii katika kuboresha maslahi yao.
Au kazi yao ni kuwabana tu
BASATA ni wazee ambao waliajiriwa siku nyingi na serikali kushughulikia mambo ya sanaa.

Sasa inavyoonekana walikuwa wanapewa mishahara tu ya kawaida na hawakuwa na shughuli nyingi za kufanya.

Sasa Kinachoonekana sasa hivi na wao wanataka pesa na kwasababu Muziki unaonekana unalipa lipa wamwamua wakomae na wasanii wa muziki.

Wewe fikiria, wale ni baraza la sanaa, ina maana nchi hii sanaa ni muziki peke yake??

Na ili wapate pesa wamejitungia kanuni zote za kudhibiti wasanii kama vile kujisajili kwao, uwezo wa kuwafungia, ukiwa na show nje ukaripoti kwao, wakague nyimbo, kufungia nyimbo n.k

Hapo lengo ni pesa tu na kujitafutia kazi za kufanya kwa lazima.

Anyway, Wasanii na serikali lao moja wanajuana
 
Yupo sahihi hajatukana
sanaa yake inalipa kodi
 
BASATA wajinga sana wanasema sheria sio mpya lakini walikuwa hawaitumii hii ni sheria wakati ule band za msondo maisha yamebadilika sana huwezi ku control japo naunga mkono nyimbo za matusi wachukuliwe na maana matusi yasiruhusiwe na nyimbo ziko nyingi unasikiliza unajuwa kabisa matusi ya wazi kabisa toka WCB na Konde. Lakini maoni kuhusu siasa iwe unasifia au hapana muhimu hakuna tusi waachie tu. Ney kapata fursa ni kama wamempa kick maana watu wengi wanataka kusikia kasema nini humo mpaka kazuiwa na yeye kachukuwa fursa. Turudi kwa Basata mtu kaanda album nzima kashoot video halafu unaenda kuchuja? ikitokea mtu katuna matusi basi fungia na piga fine kubwa tu.
 
Hawa si waliipamba CCM kwenye kampeni?

Acha nao wapambike
 
Back
Top Bottom