Nay wa Mitengo, laana ya baba ake na mihemko ya kisiasa ina mvuruga kichwa

Hujatumia akili kuchambua wimbo wa Nney. Umetumia hisia na umechambua kwa hasira na matusi kuliko Ney mwenyewe. Kwa mchango huu Ney amekuzidi akili mbali sana. Nani kakwambia elimu ni bure?

Mlinzi 5,000/= kwa mwezi kwa mwaka 60,000/= Limu 2 = 30,000/=. Walimu wa kujitolea 10,000 kwa mwezi kwa mwaka 120,000/=. Kuchapa mitihani 6,000/= kwa muhula×4 = 24,000. Chakula shuleni, michango ya Mwenge, Michango ya Mitihani ya kila wkend.

Kwa kifupi kwa mwaka 200,000 mpaka 400,000 inakutoka. Tangu JPM aondoke hii Michango ipo nasema ipoooo na lazima mtoto atoe Je? Hapo kuna elimu bure?

MUngekuwa karibu nakunasa vibao. Yaaani mijitu inaiba mali za Nchi kwa msemo wa Kulamba asali halafu taaahira moja linazuia wapuliza filimbi akina Nney? Shiiiit
 
Yaani hayo mapungufu yote ni ya Ney wa Mitego tu??

Unadhani unamchafua kumbe unazidi kumpaisha
 
shida ni ney au huku mitaani hakubiki, au shida ni promo nyingi kuliko kazi zake, au magu alituacha tunaishi kwa buku au nini, kipi hujakielewa,

usihangaike na maisha ya mtu binafsi, coz life has to begin somewhere
 
Looks like unajaribu kupindisha maana ya laana kwa kuleta maana yako.
Hapa unaonekana kabisa wewe ndiye mwenye laana, siyo huyo unayemtuhumu.

AMKA AMKA AMKA.
 
Huna akili Elimu bure ni janga Kwa TAIFA, sisi ambao tupo kwenye hii field kama wadau tunasema Elimu bure ni JANGA LA TAIFA. HAINA UBORA WALA HAIMJENGI MTU KIUSHINDANI.

NDIO MAANA WATOTO WAO HAWAPO HUKO KWENYE ELIMU BURE.

NAY YUPO SAHIHI SANA KWENYE HUO WIMBO MAANA KAONGEA UKWELI.

WE NI MPUUZII TU UNAE ITEGEMEA CCM.
 
Mimi nakuupuza wewe mleta mada kwakua wimbo nilikua sijausikiliza ngoja niutafute niusikilize.

Mnatakiwa kujifunza kuwa ofisi ya urais haina uhusiano na 'umama" , akina mama tunawaheshimu lakini hata hao kina mama pia vichaa wapo.

Rais ni public figure kama anataka asikosolewe aende kucheza na wajukuu zake huko kwao Unguja mnamlemaza sana manvyotanguliza hilo neno mama as if yupo nyumbani kwao Unguja.
 
Hata nape na boss wake wote wana laana za wazazi
 
Fungo kazini...
 
Pole sana chawa wa mama. Alichokiimba ni kweli tupu. Kama wewe ni mkweli sema hata kimoja alichoimba ambocho sio cha kweli
 
Nilisema hapa baada ya thread ya wimbo wa Ney kua tusubir povu la foma gold barid toka kwa uvccm!!
 
Umejitahidi kuandika japo na wewe unamihemko kama huyo uliesema anamihemko.
Napinga maneno yakobkwenye maandishi haya isipokuwa ya ELIMU BULE PEKEE.

Kuhusu usanii wa neyi wewe mwenyewe umeanza kwa kusema sio msanii lkn baadae ukasema ni msanii, soma maandishi yako mwenyewe.

Kuhusu kutumika na watu, wanasiasa wa upinzani na makundi tofauti sio ukweli hata kidogo, na naomba hii kasumba ikome. Kwani ney wa mitego sio mtanzania? Kwani yanayoendelea hayasikii na kuyaona? Alichosema ni mtazamo wake au nikunukuu ni ujinga wake.

Kuhusu malezi na eneo alilotoka hapo na wewe wa kukemewa kwa ubaguzi wa hali na kung'ang'ania historia za wengine.
Mfano. Diamond platinum alilelewa kwenye gongo na ujanja wa kuuza mitumba, Marehemu kanumba the same story na wao unawasemaje?

Je wanamaana kwak kwa sababu hawasemi serikali tu au wanakufurahisha na nini?

Profesa J alituhumiwa kwa ulevi uliokithiri miaka ya nyuma na ujue ulevi sio suala la kuigwa na sasa unamsifia kwa kuwa hajaisema tu serikali.

Tambua kariba za watu utajua tunatofautia kama kanisa na baa.
Tunatofautiana kila mmoja na tabia yake na hivyo tunapaswa kuchukuliana na kuvumiliana.

Awamu ya nne ya serikali yetu ilisemwa sana lkn maandiko kama haya hayakuwa kama leo.

Tujifunze kuvimiliana
Kama kundi lako limepigwa na ukaumia vumilia na wewe tafuta namna ya kuliumiza kundi hilo nao wavumilie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…