Nayachukia maisha sababu ya kifo

Nayachukia maisha sababu ya kifo

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
1,345
Reaction score
3,503
Nimeamka leo na taarifa ya msiba wa ndugu wa karibu aliyefariki jana usiku kutokana na ajali.

Umezima kama mshumaa.jpg

Kama umeshawahi kuondokewa na mpendwa wako, mzazi, rafiki wa karibu unajua maumivu makali ya kupoteza mtu ambaye alikuwepo kwenye maisha yako na ghafla hayupo tena.

Nayachukia sana maisha kila nikifikiria kuna siku nitakufa na kuwapitisha wanangu na familia yangu kwenye maumivu makali ya kunipoteza na kulazimishwa kuanza mwanzo mpya wa kuishi bila mimi 😢. Ninaishi na kitu kinaitwa "anticipatory grief" towards baadhi ya ndugu kwenye familia yangu na inanikula ndani kwa ndani.

Ulimpoteza nani kwenye maisha yako akaacha pengo ambalo halijazibika?

Tuendelee kuwaombea wote waliotangulia, wakapate pumziko, may they RIP.
 
Nimeamka leo na taarifa ya msiba wa ndugu wa karibu aliyefariki jana usiku kutokana na ajali.

View attachment 3268755

Kama umeshawahi kuondokewa na mpendwa wako, mzazi, rafiki wa karibu unajua maumivu makali ya kupoteza mtu ambaye alikuwepo kwenye maisha yako na ghafla hayupo tena.

Nayachukia sana maisha kila nikifikiria kuna siku nitakufa na kuwapitisha wanangu na familia yangu kwenye maumivu makali ya kunipoteza na kulazimishwa kuanza mwanzo mpya wa kuishi bila mimi 😢.

Ulimpoteza nani kwenye maisha yako akaacha pengo ambalo halijazibika?

Tuendelee kuwaombea wote waliotangulia, wakapate pumziko, may they RIP.
my wangu mambo😉
 
Pole kwa msiba,, nimepoteza wengi wa karibu na kuniachia maumivu yasiyoweza kuelezeka!!!

Muhimu nimejifunza kuishi yaani namaanisha kuishi nafurahia kila saa sekunde dakika kwa upendo wa Hali ya juu..... Nahakikisha napenda wanangu nawapa upendo wanaotakiwa kupata bila zidisha na kuwapa madeko.....nahakikisha familia yangu Ina furaha kuanzia mume , wanangu, ndugu zangu hapa namaanisha wa tumbo moja. Silazimishi vitu kinachowezekana nafanya kisichowezekna nakipa muda kitimie kwa wakati!.
Furaha yangu na familia yangu ndio kipaumbele changu katika haya maisha.
 
Pole na wewe pia kwa wote uliowapoteza.
Umesema vizuri sana kuhusu kuyaishi maisha kwa ukamilifu.
 
Usichukie Aunt yangu hata me juzi tumetoka kumzika ndugu yetu wa karibu, pole sana kwa unayopitia jipe moyo usichukie maisha.

Maisha yana changamoto zake nyingi huku hatma yake ikiwa ni kifo, licha ya changamoto zote bado kuna raha ya kuishi furahia wakati ulionao ungali hai.
 
Kifo kizuri sana ,unaenda kampunzika ..Hakuna mtu utashindana naye tena ,hakuna kutafuta maisha .

Kuliko kuishi kwa tabu ,wengine wana maisha mazuri wakati huo wengine wanaitwa maskini tena na kejeli juu ; utasikia masikini wana chuki sana 😅.

Bora kufa ni vile hujiamini.
 
Bora kufa tena? Wewe hauna familia au watu watakaoumia ukiondoka?
 
Tuendelee kuwaombea wote waliotangulia, wakapate pumziko, may they RIP.
Kwamba wewe ukiwa hai utende maovu halafu ukifa ndiyo uombewe na waliobaki (ambao nao ni watenda dhambi kama wewe ulivyokuwa) ili upate pumziko jema? Haya siyo mafundisho ya Biblia (kama wewe ni Mkristo). Tujitahidi kuwa na mahusiano mema na Mungu, tuombe toba na tuishi maisha yanayompendeza Mungu wakati tukiwa hai. Hii ya kusubiri ufe eti ndo uombewe na waliobaki ili upumzike salama huko uliko ni kujidanganya na kujifariji tu.

Ndugu yako apumzike salama 🙏🏿
 
Back
Top Bottom