four eyes
JF-Expert Member
- Jan 11, 2017
- 905
- 1,408
Instagram, sio Facebook au JamiiForums, ni Instagram. Hapa ndipo ambapo kila umuonae yuko very smart kimavazi, pamba kali kali na simu za gharama zipo humo katika maisha ya Instagram.
Ni humo ndipo ambapo watu wanakula maisha kwelikweli, picha za kuthibitisha za viwanja vikali na misosi mizuri ya bei mbaya imo humo Instagram.
Hakuna mwenye shida insta jamani, kila mmoja ana kazi nzuri na anaishi pazuri na anamiliki gari tena sio mkweche bali gari zuri mno la kuvutia.
Ndio huko kwenye mabinti wazuri karibu wote, sura na figa nzuri nzuri kama za kuchora utazikuta huko, rangi za ngozi za kuvutia na ngozi laini zipo huko kwa wanaotaka wake.
Kwa wenye uchu wa mapenzi madalali wa mabinti poa wapo kibao humo wewe tu, mabinti wadangaji wapo kibao na picha zao za nusu uchi zimejaa humo wewe tu.
Familia za insta ni Familia bora za mfano, ni Familia za watanashati zenye furaha, mababa na mama wa Familia insta wanapendana mno mpaka wanavaa saresare na watoto wao baba king, mama queen, mtoto prince au princess.
Hakuna stress za magu katika maisha ya insta ni full Bata na mafanikio.kuna watu wa aina tofauti kule ni jukumu lako wewe kuamua unataka kumuiga nani, kuna wale wanaojivunia uvaaji wao, kuna wale wanaojivunia bata mbalimbali mfano kina tunda, kuna wanaojivunia uzuri wao mfano kina lulu na Masogange na wale wanaoonyesha mafanikio yao na jitihada zao mpaka wakafanikiwa mfano kina masanja mkandamizaji, ni jukumu lako kuamua umuige nani uwe kama yeye.
Insta hakuna umasikini kama Facebook, insta hakuna haja ya akili nyingi na maadili kama JamiiForums, kule ni utashati, uzuri, bata na utajiri.
Ningeambiwa nichague Dunia ya kuishi ningechagua insta. Nayapenda maisha ya insta hata misiba inahuzunikiwa with class and style, kuumwa watu wanaumwa kwa style and class wanalazwa Agha khan.
Nayapenda maisha ya Insta, ndoto ya kila kijana, vipi we mwenzangu?