Ilipofika mwisho wa juma wakati wa kuiandaa sabato ulipofika, habari ikaenea uyahudi yote kuwa yule mwanamke msamaria amemwacha mumewe, kijana tajiri wa huko madale.
Furaha ikasambaa uyahudi yote kwa maana watu walijiuliza "je, yawezekanaje myahudi kumuoa msamaria? Je, haikufaa yeye kumchukua mwanamke wa ukoo wetu?"
Ndipo yule mwanamke aliyekimbilia uhamishoni kuhofia utawala wa mfalme yohana wa tano akapaza sauti yake akisema "enyi wana wa wayahudi, sikuwaambieni kuwa watu hawa watatengana? Na sasa limetimia andiko langu"
Wakati yakisambaa maneno hayo katika uyahudi yote, yule mwanamke aliyesemwa amemwacha mumewe akapita katikati ya hekalu na kusema kwa sauti kuu "ni nani aliyesema nimemwacha mume wangu, jambo hili halitakaa litokee kamwe" ndipo mafarisayo na waalimu wa sheria wakajiuliza "jambo hili lina maana gani?"
Matendo ya zari 23:2-4