Naye Rais Mwinyi wa Zanzibar Atunukiwa PhD ya Heshima Katika Uongozi Unaoacha Alama na Chuo Kikuu Cha Zanzibar (SUZA)

Hongera Rais Mwinyi unastahili tuzo hii ya Uongozi Unaoacha Alama.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar.

Chuo Kikuu cha Zanzibar kimemtunuku Shahada hiyo ikiwa ni kutambua na kuthamini Mchango wa Uongozi wake Unaoacha Alama na historia itakayokumbukwa wakati wote.

Hafla ya kutunukiwa Shahada hiyo imefanyika leo tarehe 5 Disemba 2024 katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu wakati wa Mahafali ya 22 ya Wahitimu wa mwaka 2024.

Shahada hiyo ya Heshima ya Uchumi ametunukiwa kuthamini Mchango wake na Mafanikio makubwa yaliofikiwa Zanzibar hususan Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo yaliopatikana Kipindi kifupi cha Uongozi wake wa miaka minne akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Rais Dk Mwinyi amekishukuru Chuo hicho kwa kuthamini juhudi na kazi anazofanya kwa ajili ya Maendeleo ya nchi.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amebainisha kuwa Shahada hiyo aliotukuwa Inaakisi kazi nzuri inayoifanya na Serikali anayoiongoza na itamuongezea hamasa ya Maendeleo zaidi.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameahidi kuienzi heshima hiyo na kuwahakikishia wananchi kuendelea kuwatumikia kwa uwezo wake wote na sio mwisho wa safari bali mwanzo wa hatua kubwa ya maendeleo yajayo.

View: https://www.instagram.com/p/DDNG5E_gqzE/?igsh=MTRmbTAzdW1tNWk0ag==
 
Hakika dkt Hussein anastahili kwa kazi kubwa aliyo ifanya ndani ya miaka 4. Nilifika zanzibar hivi karibuni, hakika zanzibar imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo;- Miundombinu, afya, utalii, elimu, sera ya uchumi wa buluu vyote hivyo kwa pamoja vimechochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya zenji kupaa.

Hakika Rais Hussein ni Jembe, kichwa kwelikweli, mchapa kazi kwa maarifa ya juu kabisa yaani ni mweledi asiye shaka, mwadilifu wa viwango vya juu, anaheshimu watu wote.
 
Umesikia utekaji Zanzibar? Halafu yule anafanya viitu vinaonekana. Huyu huku makelele ni mengi kuliko utendaji. Imagine hata mradi wa sgr tu hapo et mizinguo kibao
Utekaji ni upuuzi usio na msingi.

Nitajie vitu vinavyoonekana huko Zanzyna huku havionekani,Ili twende sawa.
 
Hongera Rais Mwinyi unastahili tuzo hii ya Uongozi Unaoacha Alama.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar.

Chuo Kikuu cha Zanzibar kimemtunuku Shahada hiyo ikiwa ni kutambua na kuthamini Mchango wa Uongozi wake Unaoacha Alama na historia itakayokumbukwa wakati wote.

Hafla ya kutunukiwa Shahada hiyo imefanyika leo tarehe 5 Disemba 2024 katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu wakati wa Mahafali ya 22 ya Wahitimu wa mwaka 2024.

Shahada hiyo ya Heshima ya Uchumi ametunukiwa kuthamini Mchango wake na Mafanikio makubwa yaliofikiwa Zanzibar hususan Ukuaji wa Uchumi na Maendeleo yaliopatikana Kipindi kifupi cha Uongozi wake wa miaka minne akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Rais Dk Mwinyi amekishukuru Chuo hicho kwa kuthamini juhudi na kazi anazofanya kwa ajili ya Maendeleo ya nchi.
Aidha Rais Dk.Mwinyi amebainisha kuwa Shahada hiyo aliotukuwa Inaakisi kazi nzuri inayoifanya na Serikali anayoiongoza na itamuongezea hamasa ya Maendeleo zaidi.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameahidi kuienzi heshima hiyo na kuwahakikishia wananchi kuendelea kuwatumikia kwa uwezo wake wote na sio mwisho wa safari bali mwanzo wa hatua kubwa ya maendeleo yajayo.
Kuna huyu pia 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DDNN_xcNCjM/?igsh=MTc3eWZ1YWRqeWo5ZA==
 
Back
Top Bottom