Nazeeka, naogopa!

Delegate

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2012
Posts
331
Reaction score
201
Ndugu zangu,

Nafikiri nipo katika wakati mgumu sana, nazeeka na nimeingiwa na hofu, nimegundua nauingia utu uzima, nimechukia, naogopa nahisi maisha ndio basi, kila nikipita nasalimiwa shikamoo, sipendi jamani wengine wananisalimia nawaona kama tunalingana, naogopa sana uzee.

Mvi zinabisha hodi kila kukicha, nimeanza kubadili mavazi niliyoyapenda sasa navaa kama mchungaji, sitaki lakini hakuna jinsi, mlioushinda uzee nitieni nguvu nahisi sipendwi tena nikipita hakuna anayenitazama kama zamani, naogopa kutongoza huenda nikatukanwa hadharani.

Mmh, mlioushinda uzee nisaidieni
 
Shik

Hakuna marefu yasiyo na ncha..wewe ndio ushafika kwenye ncha...Shikamoo kikongwe
 
Kuna mambo huwa hayakwepeki/hayahepukiki.

Wakti kama umeshafika, usiogope, kubaliana na matokeo.

Kwa ninavyoamini mimi, hakuna jambo muhimu kama kufurahia Maisha yako, kwa hali yoyote utakayokuwa nayo.

Kwahiyo kila hatua ya Umri utakayoifikia inabidi uifurahie, kumbuka kuna wengine hawatoweza kufikia hapo ulipofikia wewe.

Na kuna wengine ambao tayari wameshatutangulia mbele ya haki, na walipenda/walitamani sana kufikia Umri/Rika wako/lako, lakini kwa mapenzi ya Muumba hawakuweza kutimiza ndoto zao.

Haya Maisha ni mafupi sana.

Kuwa na utaratibu wa kushukuru
 
Kama sio uzee ni kifo ukiwa kijana.
Uchaguzi ni wako kifo uzeeni au changamka na moja sasa .
 
Hekima sana, maelezo yako
 
Mimi niko kama wewe ila mi nachukia kuota ndevu tu still ni kijana mdogo tu.... I wish nipate dawa ya kuzifanya zisiote arghhh 😡
 
Kubali matokeo mkuu, wala hutapata shida kuwaza uyawazayo
 
Ila unaelekea mapumziko baada ya uzee, yaani kifo au kulala, usingizi mzuri, mapumziko baada ya kuubugia upepo, maana hatukuja na kitu wala hatuta ondoka na kitu, ufurahie uzee, usio
 
Kwanini unaogopa uzee? Tuanzie hapo kwanza
 
Uzee ni vile unaamua kuishi wewe, ukiwa na hela huwi mzee!! Tafuta hela kijana utajikuta unamiaka 70 lakini ni kama una miaka 30!!
 
you just live maana hata uko kuogopa hakusaidii kitu
 

Hakuna alieshinda uzee mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…