Nazizi afa kimapenzi na producer wa kibongo...aachana na mume wake

Nazizi afa kimapenzi na producer wa kibongo...aachana na mume wake

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Hivi karibuni, mmoja wa waasisi wa hip hop nchini Kenya, Nazizi, alithibitisha kuwa ameachana ma mume wake kutoka Tanzania, Vinny, na wapo katika harakati za kupeana talaka Naziz na Vinny wana mtoto mmoja wa kiume. Msanii huyo, ambaye ni member wa kundi la hip hop la Necessary Noize, amekufa kimapenzi na Mtanzania mwingine tena, producer Herry Sappy, anayefanya shughuli zake za kimuziki kwenye studio ya Home Boyz Productions ya Kenya. Kwa mujibu wa bongo5.com, Nazizi amethibitisha kuwa na uhusiano na Herry Sappy tangu Valentine’s Day, Februari 14, na uhusiano wao ni wa dhati Chini hapa ni picha za wapendanao hao, pamoja na moto wa Nazizi na aliyekuwa mume wake.

Nazizi na Herry Sappy wakimbusu mtoto wa rapper huyo

Nazizi na aliyekuwa mumewe, Vinny, wakati mapenzi yalipokuwa

 
Dah huyo wa kwanza mzurii mweh ngoja nimtafute. kamata fursa twenzetu
 
  • Thanks
Reactions: amu
The best female Rapper ever in E.A.

Kwangu Nazizi anauwezo wa ku rap kuliko Nikki Minaj basi tu ukitokea hizi nchi zinazoitwa H.E.P.C ni mkosi dunia ya muziki kukujua.

Anayetaka abishe lakini kama unajua uwezo wa Nazizi utakaa kimya na kugonga like tu!!!!
 
  • Thanks
Reactions: amu
P.Funk,Khalifan Majani a.k.a Supadupa Producer anajua vizuri habari ya huyu dada hasa alivyochanachana biti yake kwenye ngoma aliyoshirikiana na Gangwe Mob.
 
Mambo ya kuwasumbua watoto huwa yananikera sana basi tu.
 
Mbona leo nimemsikia akikanusha hizo habari huyo Producer kwenye kituo cha Kiss Fm!
 
P.Funk,Khalifan Majani a.k.a Supadupa Producer anajua vizuri habari ya huyu dada hasa alivyochanachana biti yake kwenye ngoma aliyoshirikiana na Gangwe Mob.
Dah, umenikumbusha! Wacha nilitafute hili goma....nakumbuka funiko ambalo walifanya pale Leaders aisee.
 
Aiseee nikajua amekufa yan hayupo tena dunian kumbe kimapenzi?
 
Back
Top Bottom