Nazungushwa mahakamani kuhusu mwenendo kwa kesi yangu ya traffic nifanye nini?

co fm

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
1,541
Reaction score
2,487
Habari wadau humu JF,naomba kupata ushauri kutoka kwenu kuhusu mwenendo kwa kesi yangu ya traffic ambapo huu ni mwezi sasa toka niambiwe kesi imeisha na msababisha ajali kukutwa na hatia.

Chakushangaza kila nikienda kuchukua documents za hukumu naambiwa mara hazijasainiwa mara hakimu hayupo mara copy ya hukumu haipo. Wadau nisaidie muongozo, mimi nimepanga kwenda ngazi za juu maana haiwezekani kesi ya kitraffic nazungushwa hivi maana naingia gharama na kunipotezea muda wangu wa kufanya mambo mengine
 
mimi nimepanga kwenda ngazi za juu.

👆fuata hiyo
 
Wapelekee hela ya moto au nenda high court
 
Mkuu vumilia,nakala ya hukumu ni ndani ya siku 90 baada ya kusomewa hukumu ukipata chini ya hapo ni fadhila tu za watumishi wa Mahakama,na hizi taarifa nimezipata kwenye kipindi cha ITV sema na Mahakama, kuna mtu aliiuliza swali la muda wa nakala ya hukumu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…