NBA 2016/2017 Season Special Thread

Jibu moja MURUA sana..!
[HASHTAG]#DubNation[/HASHTAG]
 
Mkuu...
Unaonaje ukiedit huu upupu wako hapa, ili watu wasihoji UTIMAMU wako..?
Hahaha ndio maana napendaga kumbusha watu tuwe na "hakiba ya maneno". Maana ukaacha maneno yako yatawaliwe na emotions asee kesho na keshokutwa tunakuuliza "unakumbuka ulisemaje?" "vipi, unaweza kutuelezea nini kimetokea? Coz you seemed so spot on not so long ago!"
 
Hapa ni kutafuta jinsi ya kudili na KD tu, wengine watasinzia tu.
Mkuu KD ndo tatizo kubwa, hawa wengine wanapoteaga kirahisi. Klay yuko usingizini na nadhani ameshindwa kucope na ujio wa KD.
Mimi nafikiri KD wala siyo wa kuumiza kichwa...aachwe tu, ila hao wengine ndiyo wa kuwabana...anyways, coach Lue knows more, naamini atakuja na a winning game plan...
Naomba niwaulize swali moja tu watani zangu Raimundo na Nzi...hivi mmewahi kusikia kauli mbiu ya [HASHTAG]#strengthInNumbers[/HASHTAG]? Tofauti kubwa kati ya CAVs na GSW ni kwamba CAVs wanamtegemea sana mtu moja (a one man army) wakati kwa GSW ni teamwork.

LeBron akibanwa kama alivyobanwa jana, wenzake hawajui mpira wampe nani na matokeo yale ni T/O! Kyrie akipata mpira atakaa nao weeee akimtafuta LeBron na akimkosa naye atajitahidi kufanya kile akifanyacho LeBorn; to bulldoze his way to the basket!

Sasa wengine tunabaki tukijiuliza, kwani wachezaji wengine wa kuwapasia mpira hawapo uwanjani? Jana GSW walipata assists 31 ikilinganishwa na za CAVs 15, see what I mean? Kwenye lineup ya CAVS wachezaji saba hawakufunga hata goli moja, kwa GSW ni moja tu.

GSW might not be so good katika individual play but they sure know how to click as a team na ndio maana they still managed to beat a full strength Spurs in their home court and in front of their fans without KD who pulverized the much hyped CAVS last night.

Mkitaka kuifunga GSW, change your style and game plan next time you meet, la sivyo itakuwa ni kilio si hapa tu bali hata nyumbani kwenu Quicken Loans Arena...kidole kimoja hakiui chawa! GSW since playoffs is now 13-0 while CAVs is 11-2...are you still with me?

Well, this is what the world saw last night...!


Naye kocha wa CAVS Tyronn Lue anasemaje?

Cleveland Cavaliers head coach Tyronn Lue heaped praise on the Golden State Warriors after they romped to a 113-91 Game 1 win over the defending champions on Thursday night.

Speaking to reporters at Oracle Arena, Lue said the Warriors are the "best I’ve ever seen," according to CBS Sports' Sean Wagner-McGough.

"No other team has done this," Lue added, per Sports Illustrated's Ben Golliver. "13-0. They constantly break records every year."
 
Wewe mzee nafikiri unastahili kuanza kuitwa Bashite ama Magufuli unavyopenda kusifiwa. Relax, it is just one game. Nothing special; GSW have always taken game 1 in the trilogy!

Sielewi LBJ alibanwa vipi kwa kuwa na points 28, rebounds 15, assists 8 na 2 blocks. Labda zile 8 TOs ndiyo zinakufanya uone alibanwa?

Kuhusu tofauti ya assists; pengine hufahamu Cavs' basketball style. Cavs wanategemea sana isolation basketball; they don't often move the ball that much kama GSW.

Naona umesahau Cavs waliifunga GSW 3 consecutive games, hadi kupelekea GSW kumuongeza KD ili iweze kukabiliana na Cavs.

Anyways, sasa uwanja ni wako kutamba! Nasubiria J2, kisha 2 home games!
 
Wewe mzee nafikiri unastahili kuanza kuitwa Bashite ama Magufuli unavyopenda kusifiwa. Relax, it is just one game. Nothing special; GSW have always taken game 1 in the trilogy!
Sawa Mkuu, naona umeamua kutokubaliana na kocha mwandamizi wa CAVs, Tyronn Lue.

NB: Kunifananisha na Bashite/Magufuli, duh! Naomba uwe muungwana uniombe radhi. Sijali kufananishwa lakini kwa hao wawili, hapana...hapo umeniacha uchi!🙁🙁🙁
 
Hahaha watani wangu utanini.
 
Hahaha watani wangu utanini.
Ee bwana, we acha tu...yaani katika watu wote duniani kaamua kunifananisha na Bashite/Magufuli! Kwa kweli akutukanaye hakuchagulii tusi; duh, kanikomesha kweli kweli! Najua atanitaka tu radhi, Nzi ni mtu muungwana sana...

That aside, T/O za King zilitokana na kupasiwa mpira hata pale kawekwa chini ya ulinzi mkali wa maafande kama Draymond na Klay! Kwa nini yeye tu na uwanjani wako wenzake wanne? Masikini LeBron kalazimika kucheza dakika zote 40, why? Yaani kwa mechi nzima alipumzika dakika nane tu!

Kesho Jumapili waangalie sana, wasifanye makosa kama ya juzi la sivyo mzee wa watu anaweza akazimia uwanjani na hapo bado Quicken Loans Arena! Ningekuwa kocha wa CAVs, kuna wachezaji ningewapumzisha nikisubiri kuwatumia Game 3 mbele ya mashabiki wao...home court advantage.

Update...
Kocha wa CAVs, Tyronn Lue, amewataka wachezaji wake wawe more physical (watumie zaidi nguvu) katika kukabiliana na GSW siku ya Jumapili hata kama fouls zinatolewa. Ameshangaa kwa nini mchezaji kama Steph Curry hakupewa FT hata moja kwa dakika zote alipokuwa uwanjani...😵😵😵?

Rep. Barbara Lee @RepBarbaraLee
1 down. 3 to go. [HASHTAG]#DubNation[/HASHTAG] [HASHTAG]#NBAFinals[/HASHTAG]
 
NB: Kunifananisha na Bashite/Magufuli, duh! Naomba uwe muungwana uniombe radhi. Sijali kufananishwa lakini kwa hao wawili, hapana...hapo umeniacha uchi!🙁🙁🙁
Ha ha ha! Nilijua uwapendi hao viumbe! I did it purposely! Ila niwie radhi sana mzee wa GSW. Najua kufananishwa na hao waungwana ni tusi lisilo na kipimo!
 
Ha ha ha! Nilijua uwapendi hao viumbe! I did it purposely! Ila niwie radhi sana mzee wa GSW. Najua kufananishwa na hao waungwana ni tusi lisilo na kipimo!
Hata mimi nilijua hilo, asante sana...vipi leo, KD mtahakikisha hilo goti lake linadondoka au siyo...maanake niliposikia leo hakuna namna, ni ubabe tu na minguvu nikaogopa. Nakumbuka miaka ileee yaliyompata Pele wa Brazil walipokutana na Uingereza fainali ya World Cup...wachezaji wa Uingerezea walikuwa wameambiwa wahakikishe hawakosi yote, ama mpira au mwenye mpira! Duh! ilikuwa patashika uwanjani, madaluga yalipigwa hadi Pele kutolewa uwanjani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…