NBA 2016/2017 Season Special Thread

Ahahaaaaah...
Leo nimefurahi sana mkuu...
Ingawa sijaangalia game,ila vijana wamenifurahisha kwakweli...
Ila kwanini Steve Kerr huwa hapendi kuwatumia mastaa wake katika quarter zote..!?

Ukisha kuwa na uhakika na ushindi vijana inabidi wapumzike, moja ya vitu viliwachosha mwaka jana ni kukimbizana na ile rekodi ya 73/8 ndo maana kwenye playoff timu ilikuwa imechoka kinoma.

This time kocha anajaribu kuwalinda vijana na uchovu unaosababishwa na kucheza dakika nyingi.
 
Kwanini mkuu...
Rockets si waliibamiza GSW..!
Kwanini hauwaamini..!?
Ni timu zenye moto wa mabua muda wowote unaisha, ona Leo clippers wamekuwa blown out wakati wanaongoza NBA power rankings.

Naona ligi Bado haijawa shaken up vizuri contenders Bado ni wale wale GSW, Cavs, spurs labda na Bulls nadhani wana uwezo wakikaza kuliko hawa clippers, OKC, rockets
 
Mkuu Mag3
Leo naomba Steve Kerr awachezeshe mastaa wetu katika quarter zote...
Coz naona kuna kila dalili za kupatikana ile namba ya vikapu unayomuambiaga Raimundo
[HASHTAG]#DubNation[/HASHTAG]
 
Steve Kerr ameshaanza kuwatoa mastaa...
Huyu jamaa ananikera sana..!
 
A triple-double machine...ila naona Russ anafahamu fika kwamba timu yake haitofika mbali, hivyo angalau anajitahidi aambulie kitu yeye binafsi.

Eti kama energizer bunny!!! Nikikumbuka hilo tangazo, mbavu sina!
 
Hili game Knicks vs GSW Carmelo na Derrick Rose wangekuwepo lingekua tamu sana, hawapo ila madogo wanajitahidi kukaza nilitegemea wawe blown out hadi sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…