NBA 2016/2017 Season Special Thread

NBA 2016/2017 Season Special Thread

CzfbhqkUAAEGc85.jpg
 
Mie nashangazwa na hawa Lakers, juzi wamewatoa kamasi nyembamba Cleveland basket kwa basket mpaka zikiwa zimebaki dakika chache. Pamoja na kuna kipindi gap lilikuwa kubwa madogo walikuwa wanakuja tu na kupunguza kila mara na Cleveland kuongeza tena. Ilikuwa ni game nzuri sana kuangalia. Hawa madogo wa Lakers nadhani miaka miwili au mitatu kama wataweza kuwa pamoja watakuwa tishio kubwa sana ndani ya NBA.

Hili game Knicks vs GSW Carmelo na Derrick Rose wangekuwepo lingekua tamu sana, hawapo ila madogo wanajitahidi kukaza nilitegemea wawe blown out hadi sasa.
 
Wataalamu tuwekeen washind wa Leo tukampige unhind
 
Nakusalimu ndugu
Nipo ndugu yangu...tukitoka kwenye stress ya kumpigania ndugu yetu Maxence Melo tunarudi nyumbani hapa hapa, kuwashangilia the Dubs. Najua Raimundo hapendi lakini sasa tufanyeje? "Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichana", aliimba marehemu Edward Masengo miaka ya 50s na 60s...najua kwa wengi hiyo dunia ni geni kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Hahahahahahaha nimecheka mnoo.. kwamba wapo hata waliopata kuimba
 
.. kuwashangilia the Dubs. Najua Raimundo hapendi lakini sasa tufanyeje? "Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichana", aliimba marehemu Edward Masengo miaka ya 50s na 60s...

Hahahahahahaha nimecheka mnoo.. kwamba wapo hata waliopata kuimba

Heshima kwenu wakuu, kwa nini nichukie wewe kuwashangilia the Dubs mkuu?

Michezo bila upinzani si michezo, na hata hivyo mabingwa unawajua, na unajua nini waliwafanya The Dubs!
 
Heshima kwenu wakuu, kwa nini nichukie wewe kuwashangilia the Dubs mkuu?

Michezo bila upinzani si michezo, na hata hivyo mabingwa unawajua, na unajua nini waliwafanya The Dubs!
Hii Xmas si ajabu ikatukumbusha machungu yaleee...uwanja wa Quicken Loans Arena huenda ukakimbiwa tena!

sticker,375x360.u3.png

Ni hatari tupu!​
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hii Xmas si ajabu ikatukumbusha machungu yaleee...uwanja wa Quicken Loans Arena huenda ukakimbiwa tena!

sticker,375x360.u3.png

Ni hatari tupu!​

Ha ha ha, sasa nakumbushwa machungu yapi?

Hayo ni matokeo ya game ya mwisho kukutana hapo Quicken Loans Arena.

Last Game at Quicken loans Arena.jpg
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapana nakumbuka hii...!

ah_recap_warriors.jpg

Okay, naona umeamua ukumbuke zile za zamani sana, sisi kwa tunakumbuka hizi za mwisho kukutana.

Na mwaka huu na sisi tunakuja kusikiliza kama harufu ya shampeni bado ipo pale Oracle.
 
Antetokounmpo aka Greek Freak atakuja kuwa bonge la star, make namwona anasumbua sana sana.

Na leo inabidi game iishe mapema ili tujiandae na X-Mass, siyo kuchoshana mpaka OT.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yaani ile Le Bron kukaa bench jamaa wanapunguza gap kama la 10 points.

Duh!
 
Yaani ile Le Bron kukaa bench jamaa wanapunguza gap kama la 10 points.
Duh!
Kama kuna mchezo nimeufurahia ni wa jana kati ya Warriors na Nets. Mpaka HT Nets walikuwa mbele kwa 65-45 na kila moja akawa anasema leo Warriors wamelala! Cha ajabu ni kwamba mimi hata sikuwa na wasi wasi lakini mwenzangu akanikumbusha pengo la kukosekana kwa Green.

Nikamuuliza kama amewahi kusikia kaulimbiu ya GSW ya [HASHTAG]#strengthinnumbers[/HASHTAG]. Nikawaona Curry na Kd wanajadiliana kama vile wasimuangushe ndugu yao ambaye kajaaliwa mtoto wa kiume. Na kweli walilofanya Warriors kutokea hapo, wapenda NBA hawatakisahau!
 
Kwa wapenzi wa NBA msisahau leo mchapo wa nguvu repeatition ya 2016 NBA Finals kati ya CAVS na Warriors kuanzia 11.00pm EAT. Kwa maoni yangu pamoja na Warriors kumpata KD lakini CAVS wanaonekana tishio zaidi mwaka huu kuliko walivyokuwa msimu uliopita ulinganisha na GSW.

Sijui kukosekana kwa JR leo kutawaathiri vipi CAVS. Huyu kafanyiwa operesheni ya kidole gumba cha mkono wa kulia na inasemekana atakuwa out for 14 weeks.
 
Nadhani kwa kipindi JR atakuwa nje atapumzika na kurudi na nguvu mpya , make trend yake haikuwa nzuri sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom