Hii ndiyo NBA bana, maana timu zilizokuwa zinapewa nafasi ya juu kutwaa Ubingwa naona zinatolewa moja baada ya nyingine. Magic wakipoteza game zote 2 wajue ndo wameondoka, wakienda TD Garden wanaweza kushinda game moja tu.
Kuna mambo mengi, ama walijiamini sana kwa kuwa kwenye regular season walishinda games 3 kwa 1, lakini gap la points lilikuwa dogo sana na huwezi ku-conclude kwamba aliyeshinda games nyingi kwenye regular season ndo atashinda kwenye playoffs.
Timu walizokutana nazo kwenye round ya kwanza na ya pili, zilikuwa mayai. So walikuwa na over confidence kwamba Celtics akija wangembanjua. Pia kukaa wiki nzima inaweza kuwa ilichangia.
Ngoja tuone hii series itaishia wapi. But game ya leo inaweza kuamua kama itakuwa ni series ndefu ama fupi.