NBA Playoffs 2009/2010: Where's Your Money At?

NBA Playoffs 2009/2010: Where's Your Money At?

If both the Celtics and the Lakers advance, there will be a lot of BIG MEN on court! Expect something VERY PHYSICAL!
 
kwa mwendo huu sidhani kama hata lakers watatoka kwa celtics

Duh,huu sasa utani..

Celtics ni wazuri ila sioni kama wata-compete kivile na mabingwa watetezi. Timu pekee iliokuwa na potential ya kumatch up na LAL walikuwa Thunder na KD. Kwa maoni yangu LAL raundi iliopita na hii na Suns naona hakuna wa ku-match nao all the way. Naweza kukosea maana matokeo ya nyuma yanadanganya sana, nilidhania Magic wanaeza kuwadhibiti kirahisi Celtics au Cavs kwa jinsi walivokuwa wakitoa dozi ya 4-0 kwene raundi zilizopita na hata kwene regular season walikuwa pazuri statisticalwise, lakini sio, huenda kila timu ina mbabe wake bana.
 
Mkuu Abdulhalim

Wakati mwingine NBA huwa haitabiriki kirahisi. Kutumia statistics za regular season kama indicator ya performance nayo inaweza kuwa wrong. Timu zikishaingia kwenye playoff stage huwa zinabadilika sana na hata intensity ya game huwa inabadilika kwa kiasi kikubwa. Mfano, Dallas na Denver walikuwa wanapewa nafasi kubwa kwamba ndo wangeichachafya LAL, lakini wametolewa. SAS waliingia kwenye playoff kwa hatihati, lakini wakaja kumtoa Dallas round ya kwanza.

Kwa upande wa Western Conference, round ya kwanza ilikuwa na competition kali kuliko round ya pili. Round ya pili hakukuwa na ushindani, series zilikuwa fupi sana na ndiyo maana LAL na SUNS wamepumzika wiki nzima.

Mimi ni shabiki wa LAL, lakini sina uhakika sana kama LAL wanaweza kuchukua ubingwa nikiangalia physicality na intensity ya game ya Celtics, just in case finals ikiwa ni LAL vs Celtics. Hapo chances ni 50-50.

Kwa upande wa LAL, Andrew Bynum anaweza asicheze dakika nyingi sababu ya goti, so ni advantage kwa C's kwa kuwa Perkins atakuwa na Odom ambaye kwa physicality wanaweza wasi-match. Gasol anaweza ku-match na KG. Wallace ni mchezaji mchafu sana, akiingia kazi yake ni foul na ku-intimidate offense ya timu pinzani. Game ya kwanza alimnyanyasa sana Howard mpaka kijana akawa frustrated. Kobe anaweza kwenda na Ray Allen, PP anaweza kwenda na Artest. Kasheshe iko kwa Rondo, huyo dogo ni balaa, sina hakika kama Fisher anaweza kumdhibiti, labda wabadilishane kama ilivyokuwa kwa OKC Thunder. Maana Westbrook alimnyanyasa sana Fisher kiasi kwamba Kobe akajitolea kumdhibiti. Tatizo jingine, Kobe akianza kumdhibiti Rondo, hapo lazima ujue kwamba offense ya LAL inakufa.

Ukija kwa upande wa bench, LAL the only guy wanaemtegemea sasa ni Odom. Brown na Farmar hawako consistent na hata Odom nae hayuko consistent sana. Kwa upande wa C's, Tony Allen na Glen Davis wamekuwa wakisaidia sana pande zote mbili offense na defense, bado kuna Wallace ambaye ni defender wa big men, na anaweza ku-shoot long and medium range.

Kwa hiyo kama LAL na Cs wataingia kwenye finals, series inaweza kuwa ngumu na ndefu, tuombe Mungu LAL wasije wakapoteza home-court advantage kama Magic walivyoipoteza yote kabisaaaaaaaaa.
 
Game ya leo itatoa mwelekeo wa LAL, iwapo wakishinda basi matumaini ya kucheza Finals yatakuwa makubwa, lakini wakipoteza, hapo patakuwa pagumu, tunaweza kuwa na series ndefu sana.
 
leo game tight kidogo,SUNS needs to make few stops
 
Niliacha kuangalia baada ya kipindi cha kwanza, duh ngoma droo sasa.
 
Lakini nadhani Lakers watashinda....my gut feeling...I can just sense it
 
Lakers watashinda coz Suns hawana D-E-F-E-N-C-E
 
wakulu hishma nyingi kwenu.mbona kumekua kimya ghafla apa(labda huko mliko ni usiku sana now) but ki-ukweli hapa hua kama naona game live(coz ka-DSTV kangu kamekatwa,sijalipa bana so sipati hata zile chache kwa espn).tasavali bandugu,update me jameni!
 
wakulu hishma nyingi kwenu.mbona kumekua kimya ghafla apa(labda huko mliko ni usiku sana now) but ki-ukweli hapa hua kama naona game live(coz ka-DSTV kangu kamekatwa,sijalipa bana so sipati hata zile chache kwa espn).tasavali bandugu,update me jameni!

lakers 2--suns 0
celtics 2--magic 0
 
Mabingwa watetezi hawana mpinzani mpaka dakika hii. Labda bunduki zao zipate ajali hapa katikati.

mkuu mi bado naamini C's ni tishio kwa Lakers
cheki match up
Rondo vs Fisher
R.Allen vs Black Mamba
Pierce vs Artest
Gannet vs Gasol
Perkin vs Bynum

Sasa ukiangalia hizo match up KOBE tu ndio atashinda kwa Lakers, na C's hawatajali hata KOBE afunge 40pts lakini WATAHAKIKISHA HAWA SUPPORTING CAST HAWAFURUKUTI kama wanavyowafanya Magic.
 
Who now doubts that this is Boston's series? We are heading to the final. I'm going to go ahead and predict a sweep.
 
Back
Top Bottom