NBA Season 2015 - 2016: Special thread

Thanks be to good old weather, even the Andys are coming out to have a sniff of fresh air! It must have been stifling inside. Well, enjoy it while it lasts...you never know when it will start raining cats and dogs again. Never trust the weather dude!
vivid hallucinations

kwikwikwi
 
Mag3, Tyta, Steph Curry, Alegria do povo, King Shaat, Mazigazi, shansarie na wapenzi wengine wote wa GSW nakupeni pongezi kwa kipindi chote cha hii series, kabla haijaanza nilikuwa na uhakika wa kuwafunga mapema, mkatufunga 2 bila, then 3-1 nikarusha taulo uwanjani, bahati mbaya taulo likanasa kwenye moja ya nguzo za ulingo, hivyo haikufika uwanjani.

Natangaza rasmi kuliondoa lile taulo pale kwenye ulingo, which means nimefufua tena kwa asilimia 78 uhakika wa mimi kushinda game 7, naomba kutangaza rasmi bila kificho kwamba bingwa wa Mwaka huu ni Cavs, Finals MVP sihitaji kumtaja.

Ni masikitiko makubwa kwamba timu inaweza kuwa na ushindi wa 73-9 huku ikiwa na unanimous MVP ikashindwa kuchukua ubingwa.
 
Lakini pia mpunguze kulia lia.

Series hii mpaka muda huu imeonesha utofauti mkubwa kati ya uchezaji wa ki-netball na ki-basketball.
 
Nyani Ngabu ngabu una point sana kuna watu wanasoma mitandaoni tu hata mechi hawaangalii... na mengine hawaelewi waliyosoma ila wanajiandikia tu..

Jamaa huwaga ana imaginations za ajabu kweli.

Anapenda sana kutoa kauli za jumla jumla.

Na nadhani kuna mambo huwa anasoma lakini hata haelewi anachosoma.
 
mvp mcheza netball anaruka ruka tu... badala ya kuibeba timu yeye analalamika tu na mkewe...

hadi bench players wanacheza vizuri kuliko mvp...

mara nyingi drymond green anaisaidia warriors kuliko mvp


 
mvp mcheza netball anaruka ruka tu... badala ya kuibeba timu yeye analalamika tu na mkewe...

hadi bench players wanacheza vizuri kuliko mvp...

mara nyingi drymond green anaisaidia warriors kuliko mvp

Hajawahi kucheza vizuri kwenye finals, ni mzuri regular season ambayo hakuna kukabana kivile.
 
[emoji14] [emoji14] [emoji14] [emoji14] [emoji14] Raimundo I guess u've been forgetting who are competing with u .Is the #warriors.

I would like to see the sportmanshi p farewell after the end of the series ,whether we'll win or you'll.

Take a pow [emoji109] wait for the bitter end[emoji28]

#strenghinnumbers[emoji123]
 
Hajawahi kucheza vizuri kwenye finals, ni mzuri regular season ambayo hakuna kukabana kivile.
Hajawahi kucheza vizuri kwenye finals, kwani hizi ni finals zake za ngapi?? Regular season hakuna kukabana ina maana post season ndio kuna kukabana sio??

His post season stats stands at 33.8 Minutes, 25.6 Points with 5.4 Assists.. Game 3 za mwisho kwenye series za OKC alifunga 31 Points, 31 Points, 37 Points consecutively.. Game 3 za mwisho kwenye series hizi za Cavs amefunga 38 Points, 25 Points, 30 Points..

Post season ya 2014/15 stats zake ni 39.3 MPG, 28.3 PPG, 6.4 APG.. Game 3 za mwisho against a team ulikuwa unaisifia kwa defense mwaka jana Memphis alipiga 33, 18, 32... On Western Finals akapiga 40, 23, 26.. Na finals mkiwa 2-1 game 3 za mwisho akawapiga 22, 37, 25... Kumbe hizo ni stat za mtu anayecheza Netball?? Kumbuka game 4, the most important game for Cleveland to tie things up, Curry showed up on your court and score 38 points on 40 Minutes ila Lebron alifunga 25 points in 46 Minutes ila hakuna aliyemshambulia Bron.. Hizi game zina on and off nights.. Curry si Mungu ajiamulie tu kila siku awe anacheza vizuri. Hata mchezo wa jana alicheza vizuri tu ila tatizo lilikuwa foul trouble tu..

Mnachofurahisha zaidi ni Lebron akifungwa basi yeye amekosa msaada/teammates wa kumsaidia ila Curry akishinda basi yeye anabebwa tu na teammates hana chochote, ila wakati huo huo Curry akishindwa basi lawama zote ni kwa Curry. Sasa swali langu, kama GSW inaposhinda Curry hapongezwi kwa chochote ila mnasema amebebwa na watu fulani, sasa kwanini ikishindwa mnamshambulia Curry???
 
Leo leo leo. ... leo nakuunga mkono, mguu na shingo nakupatia boss. You nailed it.
 
Leo leo leo. ... leo nakuunga mkono, mguu na shingo nakupatia boss. You nailed it.
Hizi chuki hizi, acha tu... Wengine wanasema Curry hastahili kusifiwa sababu katokea familia ya kitajiri ila Lebron ndiye anastahili sababu ametokea familia maskini na ilibakia kidogo tu angekuwa homeless kid..
 
Lebrons Post season stats for 2015/16 are 38.8 Minutes with 26.3 Points to go with 7.5 Assists.. Sasa hizi Stats zina tofauti ipi kubwa na Curry?? Na hapo ni Lebron kacheza 5 Minutes zaidi ya Curry..
 

Nimekusoma mkuu, nilitaka kumaanisha hajawahi kuwa MVP wa Finals na hatakuwa mwaka huu hata kama timu yake ingeshinda.

Nadhani nitakuwa nilitumia maneno tofauti na nilivyotaka kumaanisha, so far sibishani na ulichokiandika na nadhani hata wewe hutabishana na mimi juu ya Curry kutokuwa Finals MVP.
 
Kwanini asiwe kama game 7 atafanya kama alichokuwa anakifanya regular season?? Mpaka sasa nani kwako kutoka Warriors unaona yuko favorable kupata Finals MVP bila ubishi?? Kwa Cleveland anaonekana ni Lebron kama watashinda.. Ila kwangu mimi naona ni bora apewe Klay najua atakuwa moto sana game 7..
 
Lebrons Post season stats for 2015/16 are 38.8 Minutes with 26.3 Points to go with 7.5 Assists.. Sasa hizi Stats zina tofauti ipi kubwa na Curry?? Na hapo ni Lebron kacheza 5 Minutes zaidi ya Curry..
Mwenzako anaongelea NBA Finals series, na siyo postseason yote. Finals' MVP hapatikani kwa kuangalia michezo yote ya postseason; wanaangalia umekuwa na umuhimu na thamani gani kwenye timu yako.

So far Curry, kama unanimous MVP haja-live to the stand of being the 1st unanimous MVP. The Finals ndiyo the biggest stage kwa MVP kuonyesha kwanini yeye ni MVP. Curry ameshindwa (so far) ku-prove yeye ni MVP kweli at the biggest stage, tofauti na akina MJ na Bron ambao wamewahi kuwa regular MVPs na Finals' MVPs. At the biggest stages, Curry amekuwa aki-choke: cheki All Stars games (mara 3 alizocheza) ameshindwa hata kuwa MVP hata mara moja?!? Ndiyo maana sisi humu tunamsema sana; ingawa media powerhouses (haswa US) zinalipotezea (hili la kuto-live to the 1st unanimous NBA MVP) kwa sababu ni kipenzi chao, wanachotaka kiwe mfano kwa watoto wao. Wakifanya hivyo (kum-toast na kum-blast) watawavunja mioyo na kuwakatisha tamaa watoto wanaoelekezwa waige mfano wa Curry.
 
Hadi All star?????????? Kwahiyo Westbrook aliyeshinda MVP ya all star alifanya nini kwenye NBA Western Conference finals? hebu toa hiyo Category hapo kumpima mtu aiseeee.
 
Hizi chuki hizi, acha tu... Wengine wanasema Curry hastahili kusifiwa sababu katokea familia ya kitajiri ila Lebron ndiye anastahili sababu ametokea familia maskini na ilibakia kidogo tu angekuwa homeless kid..
Braza uwa unasoma na kunielewa kweli? Au ndiyo tatizo la comprehension alilolisema Ngabu nawe unalo? Ni wapi nimesema Curry hastahili kusifiwa kwa sababu anatoka familia ya kitajiri? Hivi ndivyo ulivyoelewa kile nilichokiandika?

Nilichokisema ni kwamba historia ya Curry ya kupata 'mafanikio' ndiyo inatengenezwa kuwa ndiyo sahihi kwa vijana kuiga. Kwamba Curry anafaa kuwa mfano wa kuigwa 'role model' kwa vijana wa kimarekani. Kama unaelewa hili suala kwa context ya Marekani, nafikiri itakufanya uelewe kwa wepesi ninachokisema. Bad boys kama kina Bron, RW na hata Durant, uwa hawapaswi kuwa role models wa watoto wao (wa the establishment). Ila good boys kama akina Curry na Klay ndiyo wanapaswa kuigwa. Kama unaelewa nguvu ya media powerhouses kwa Marekani (katika kutengeneza 'heroes' and 'villains') pia utanielewa haraka. Hivyo hilo la Curry kuwa 'good boy' anayepaswa kuwa role model limemfanya asiwe akiwa-blasted na toasted na media. Ndiyo maana, kama nilivyosema huwezi kusikia media powerhouses wakimsema vibaya 'good boy' wao ili wasiwauzi watoto wao wanaopaswa kujifunza kutoka kwa Curry. Hiki ndicho nilichokisema. Yeye asifiwe tu, ila akosolowe pia kama ambavyo akina Bron, RW na Durant wanavyofanywa.
 
Hadi All star?????????? Kwahiyo Westbrook aliyeshinda MVP ya all star alifanya nini kwenye NBA Western Conference finals? hebu toa hiyo Category hapo kumpima mtu aiseeee.

All great players (MJ, Bron na KB) wamewahi kuwa All Stars MVP. Hii imekaa kwenye CV zao. Westbrook siyo among the GOAT; hapa namwongelea Curry ambaye media inajaribu kumweka kwenye platform moja na GOATs. Sasa anashindwa hata kuwa MVP wa All Stars kweli?
 
It's only his third all star and you guys tripping like he's played 7 or 15 like the one you've mentioned.. Hebu acheni double standards hizi aiseee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…