Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lamar Odom is in... Gary Payton maaannnnnn.... It's emotional....
Kobe scored 60 in his last game, then GSW has a 73-9 record. A great day for Basketball fansKOBE'S FINISHING LINE..... AND WHAT CAN I SAY? MAMBA OUT
Mkuu, kwanza karibu...najua tunakubaliana kwa mengi lakini kwa hapa lazima tutofautiane kidogo. Nilikuwa shabiki mkubwa wa Da Bulls miaka hiyo na hakuna mchezaji aliyenikosha kama MJ lakini lazima tukubaliane kwa jambo moja...vijana wa Warriors wameleta kitu kipya kabisa katika mchezo huo haukuwahi kuonekana.
Hata aliyekuwa kocha wa Da Bulls, Phil Jackson, ambaye mwanzoni alisita kukiri umahiri wa hao vijana taratibu, baada ya kujikuta yuko peke yake huku rekodi zikizidi kuvunjwa, kasalimu amri. Ukisoma tweets za watu kama Scottie Pippen na Magic Johnson, wote wanakiri kuwa kwa mchezo wa GSW, Ba Bulls wangepata shida sana.
Kitaalamu na kiteknolojia ni kama kulinganisha analogue na digital.
Mkuu BAK za masikuuu!!!Mkuu Mag3 hapa acha tutofautiane, ile NBA ya 90s kamwe huwezi kuifananisha ni hii NBA ya usiniguse ya 2016. Refa walikuwa wanaacha wacheza wafanye yao hawa nare nare wa GSW wasingeona ndani kwenye NBA ya miaka ile. Kuna timu ambazo zilikuwa zinamkamia Michael Jordan and Da Bulls timu za East na West. Playoffs ilikuwa ni habari nyingine pale Da bulls ilipokutana na timu za East hasa Detroit Pistons "Bad Boys" New York Knicks, Cleveland na hata Miami Heat. S Curry na Klay Thompson na wazuri sana kwenye hii NBA ya 2016 soft NBA lakini ile NBA ya undava undava ya 90s wangepambana na Da Bulls kwenye finals sidhani kama hata wangeshinda game hata moja.
Mkuu BAK za masikuuu!!!
Mkuu pamoja na kwamba kila mtu ana haki na mawazo yake, ila naona huitendei haki GSW. Hata game moja wasingeshinda???.
Kuna article moja iko ESPN wamejaribu ku'pit timu hizi mbili katika kila scenario...yani nani angeshinda kipindi kile, nani angeshinda kipindi hiki, na factors zingine, etc. Ntaileta huku. Na wachambuzi wamekuwa makini kutokuwa biased na "heat-of-the-moment" na "old glory of yore" na kutoa facts ambazo kwa kiasi flani unaridhika kuwa watu wanaweza kuwa wakweli na with fair judgemental.
Ila hata game moja?!? Nah bro.