GSW imeingia tena kwenye lile kundi lililo-defy odds kwa kuwageuzia kibao OKC, from 1-3 to 4-3! Ni timu chache sana zilizoweza kufanya hilo na fundisho hapa ni kwamba kwa Warriors it ain't o'er til it's o'er. Historia ya GSW itakapoandikwa itakuwa na mengi mapya lakini la msingi litakuwa ni jinsi walivyoweza kui-revolutionize mchezo wa Basketball!
Kwa mara nyingine chuki za Barkley kwa Warriors zilijidhihirisha alipotamka kwa mdomo wake kuwa OKC wangeitoa Warriors katika mchezo wa jana. Ningekuwa yeye ningeachana kabisa na hizo tabiri zinazokufanya uonekane juha kabisa asiyejua hata anachoongelea! Ni aibu kubwa kwa hall famer kujidhalilisha kama anavyofanya Charles Barkley!