Licha ya mapungufu ambayo yanaweza kuwa ya kimfumo [systematic] katika hili, nadhani ni vema pia tuangalie upande wa watahiniwa wenyewe wa mitihani husika. Wengi wa watahiniwa [hasa wa final stage modele E and F] ni wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu. Hawa ni watu ambao wakiwa vyuoni husoma semester moja kwa wiki 15, hupimwa kwa Coursework pamoja na final examination, tena examiner anakuwa yule yule ambaye hufundisha, hivyo ukimjulia angle anazopenda tu umefaulu. Lakini haishangazi kuona mtu ana supplementary moja au mbili kwa semester.
Anapofika kwenye mitihani ya NBAA:
Kwanza: anayetunga/sahisha mtihani si rahisi kutokea coincidence kuwa ndiye aliyemfundisha
Pili: Syllabus [at least for core subjects in the final stage] inashauri mtahiniwa apate 9 months of full time training ili aweze kufanya mtihani. Most of us tumefanya 3 months of weekend/evening trainings.
Tatu: Hata hizo weekend/evening training tunahudhuria tukiwa tumeshachoshwa na waajiri, na pia mahudhurio yanakwamishwa na foleni, vikao vya arusi, semina za kikazi, n.k.
Nne: watahiniwa wengine hawafanyi kazi za kihasibu maofisini mwao hivyo wanaishia kukariri
Sasa tujiulize, Je wakifeli tushangae??, mie naona hata hiyo 16% iko juu sana.
Naomba kuwasilisha!!