NBAA inatakiwa kuchunguza madai ya Kigwangala na kama yana ukweli kuwafutia leseni ya kufanya auditing wahusika

NBAA inatakiwa kuchunguza madai ya Kigwangala na kama yana ukweli kuwafutia leseni ya kufanya auditing wahusika

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Posts
11,966
Reaction score
11,218


Auditing is a profession na trustworthy ya report is key to stakeholders.

Iwapo madai ya Kigwangala yanaukweli upande wake aujachunguzwa na control measures za matumizi ambazo ahusiki nazo kuamua matumizi.

Wahusika wa hiyo report wamevunja kanuni za auditing ethics and obligations, makosa ambayo wanatakiwa kuvuliwa practice certificate kwa miaka kadhaa.

=====

Mbunge wa Nzega Vijijini Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla ametoa ya Moyoni baada ya kukutana na Waandishi wa Habari katika Viwanja vya Bunge kuhusu sakata lake alivyokuwa Waziri wa Utalii na Maliasili na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Ripoti ya CAG aliyoifanya Jijini Dodoma mwaka jana (2021), alisema katika Wizara hiyo ya Utalii na Maliasili kulikuwa na viashiria vya abadhirifu wa Fedha kutokana na kanuni mbalimbali kukiukwa.

Jioni ya leo Dkt. Kigwangalla, aliwaambia Waandishi wa Habari kwa muda mrefu alikuwa kimya kwa kuheshimu, sasa hata nyamaza anaweka wazi tuhuma zilizokuwa zinafanywa juu yake
 
Kigwangala ni mwizi mzoefu
Aina maana hana hoja auditing inatakiwa kuwa fair and not misleading kama mtu ahusiki na kuhidhinisha matumizi ukimtuhumu ivyo ni kosa kwenye professionalism.

Hao NBAA if they’re serious kwenye role yao as practice regulators this is a case study. Hayo ya serikali wawaachie wenyewe lakini ya professionalism na kusimamia quality ya kazi ni wao.

Kwa ili Kigwangalla ana hoja za msingi, kwengine duniani muhusika unazuiwa kufanya kazi accounting kwa tuhuma kama hizo.
 
Kigwangala anendeleza tabia ya viwaziri vya CCM kukataa dhamana. Anajivuaje dhamana? Yaani yeye akae pale, manunuzi yafanyike, halafu ajiondoe kwenye dhamana?
Mbona kaelezea kuna system za kuidhinisha matumizi ambazo yeye hana mamlaka nazo. Pamoja na kuwaambia CAG they did not bother to verify that.

Hiyo taasisi inaanza kupoteza uaminifu wa kazi zake kama utamaduni wao ndio huo.
 
Sasa hapo ni NBAA au tume huru iundwe Ichunguzwe maana CAG ni mtu mkubwa Sana hawezi vhunguzwa na kataasisi kadogo kama hako
 
Ssa hapo ni NBAA au tume huru iundwe Ichunguzwe maana CAG ni mtu mkubwa Sana hawezi vhunguzwa na kataasisi kadogo kama hako
Tume huru hayo ni ya serikali kwa upande wao.

Alikadhalika NBAA inajukumu la kulinda quality standards za kazi kutokana na mapendekezo ya professional bodies on how work is to be done and code of conducts.

Na kama kuna makosa NBAA wanaweza ondoa jina lako kama qualified individual ya kufanya auditing. Hayo ys serikali na wenyewe wanataribu zao.

Ila kwa upande wa NBAA as a regulator this is serious breach of practice.
 
Kigwangallah ni mpuuzi,kachezea fedha za TANAPA & NCAA hadi zikaamriwa kupelekwa Hazina.
 
NBAA wamejaa akina meku na manka.

Lazima walikuwa wanambeba Professa na kumfitini Daktari Kigwangalla!
Sio swala la ukabila issue ni CAG report

NBAA ni regulator wa viwango vya kazi zote za uhasibu Tanzania.

Moja ya majukumu yao ni kusimamia international standard za kazi zinazopendekezwa na bodies za kimataifa kama ‘International Auditing and Assurance Standard Board’ (IAASB) ambao wanatoa muongozo wa procedure standards za kufuata kwenye auditing.

Sasa ukimsikiliza Kigwangalla hapo na kwa mujibu wa ISA (International standards of Auditing) regulation 720 ambayo inasema kama inconsistency za maelezo na matumizi ni jukumu la auditor husika kutatua ilo tatizo either akague control systems or doing other auditing verifications, kabla ya kutoa report. Na Kigwangalla kaweka wazi yeye hana mamlaka ya kupanga wala kuidhinisha sehemu kubwa matumizi kama inavyodai, sasa auditor kajiridhisha na ilo kabla ya kumtuhumi.

Ni wazi auditors husika wanavunja professional codes of conduct na kuja na manufactured report, hayo majukumu ya serikarini majungu ya wana siasa wawaachie wenyewe na uchunguzi wao.

Ila NBAA kama msimamizi wa viwango vya kazi za uhasibu anatakiwa awachunguze wahusika kama wanafuata auditing standard this is a serious professional breach nchi zingine unafungiwa kufanya kazi za uhasibu kabisa.
 
Hamisi Hamisi mbona unapenda sana uwàziri ,ccm hebu mtuambie huyo Hamisi yupo ukurasa wa ngapi wa ilani yenu ya uchaguzi 2020-2025 ambayo bila Hamisi mnakwama maana kila siku Hamisi Hamisi mara unaibu spika Sasa Vita na CAG
 
Back
Top Bottom