Nbc bank imekufa....

Nbc bank imekufa....

notifeki

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2013
Posts
402
Reaction score
283
Wiki mbili zimepita tangu nijaze fomu kufungua account NBC nikaambiwa nisubiri ikiwa tayari watanipigia simu. Nimesubiri mpaka nimechoka kwani nilikuwa nategemea kutumia account hii kutumiwa hela yangu ya mkopo ambao upo tayari. Kuna tatizo gani nbc? Mbona bank zingine unafungua account dakika chache tuu inakuwa active. Wiki mbili kufungua account? Nawashauri jamani msijipeleke kwenye benki hii ni aibu tupu. Nilikuwa sifaham. Kumbe wanaosemaga nbc kumejaa vilaza kwa ajira za kujuana hawajakosea. Yaani libenki libovu ajabu sikutegemea. Pumbaaaaavuu kabisa.
 
NBC is the worst bank in the history of existence. I thoroughly hate them.
 
Mkuu badilisha heading ya uzi!
Maana taarifa iliyoko ndani ni tofauti na heading!
 
Si utafungua hapo pa. Dakika mbili?
Nakubaliana na wewe inaelekea kufa maana hata mikopo hawatoi toka mwaka uanze wanamatatizo ya mtaji BOT
 
Si utafungua hapo pa. Dakika mbili?
Nakubaliana na wewe inaelekea kufa maana hata mikopo hawatoi toka mwaka uanze wanamatatizo ya mtaji BOT

Taratibu jamani mtatupandisha pressure!
 
Benki hovyo kabisa. Kweli mswahili hawezi kuongoza benki
 
Nasikia tatizo jingine kubwa ni kuwa wafanyakazi hawako motivated kabisa kwani kuna tetesi kuwa kuna redundancy inakuja kama ile ya barclays tanzania, hii ni kwa sababu barclays london wamenunua shares za absa hivyo barclays london ina i control kwa kupitia mlango wa nyuma nbc. Hilo la kuajiri kwa kujuana nasikia nalo lipo pia sana na kuna mfano wa kitengo chao cha sheria ambako wana sheria karibu wote wa zamani wameondolewa na kuletwa wapya kwa kujuana na mkuu wa kitengo hicho. Yaani wanaiua hii benki yetu kongwe, inasikitisha kwa kweli.
 
Ndio maana mafuru katema mzigo soon utasikia naye kala shavu kama rished bade
 
Wiki mbili zimepita tangu nijaze fomu kufungua account NBC nikaambiwa nisubiri ikiwa tayari watanipigia simu. Nimesubiri mpaka nimechoka kwani nilikuwa nategemea kutumia account hii kutumiwa hela yangu ya mkopo ambao upo tayari. Kuna tatizo gani nbc? Mbona bank zingine unafungua account dakika chache tuu inakuwa active. Wiki mbili kufungua account? Nawashauri jamani msijipeleke kwenye benki hii ni aibu tupu. Nilikuwa sifaham. Kumbe wanaosemaga nbc kumejaa vilaza kwa ajira za kujuana hawajakosea. Yaani libenki libovu ajabu sikutegemea. Pumbaaaaavuu kabisa.

Unashangaa nini? Miafrika ndivyo tulivyo, (Nyani Ngabu, 2007,2008,2009,2010,2011,2012,2013)
 
Enibisii si ndugu yake Mama moja na Bakileis? mama yao si ABSA ya Sausi Afirika? au haijabinafisishwa? au kuna ajenda ya kuongusha makusudi by wamiliki wake wa Sausi? sina nia mbaya nao, ila isijekuwa inafanyiwa kama Eya Tasania
 
NBC haijafa acha kudanganya watu. Suala la huduma mbovu ni tatizo kwa makampuni karibu yote ya Tanzania, tena bora hata hao NBC ulipata hata mtu wa kukupatia hizo form, kuna sehemu zingine unaenda na haraka zako unakutana na mhudumu anakutolea mimacho tu utafikiri uko uchi... it's boring kwa kweli.
 
Duh kweli wewe una bahati mbaya, kiukweli nina account bank nyingine.....lakini kamwe siwezi funga account yangu ya NBC. Hii benki kongwe nimetoka nayo mbali sana, haya matatizo madogo madogo ya huduma yana sovika kirahisi tu. By the way ni matatizo yaliyopo hata kwenye benki nyingine pia.
 
Back
Top Bottom