NBC Bank Operation Department Huduma Mbovu

hekimatele

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2011
Posts
9,890
Reaction score
2,795
Wadau leo naomba niweke kero zangu nilizozikusanya over the past few months including today.
Huduma zitolewazo NBC kwa kweli si za kuridhisha hususan Corporate Branch hapo Baharini Posta. Kwanza kuna madirisha ya teller si chini ya kumi ila cha kushangaza ukiingia ndani unakuta aidha teller wawili au watatu tu ndo wanaotoa huduma kwa takriban zaidi ya watu 50 na zaidi walioko kwenye queue ambayo inaongezeka kila inaposogea dakika moja.
Ukiuliza unaambiwa wameenda lunch hususan kama umeenda mida ya mchana ila cha kushangaza unaweza kukaa zaidi ya masaa mawili kwenye queue na wasirudi huko lunch.
Leo kilichoniudhi zaidi nimefika saa 8 mchana huu hakuna umeme na hakuna jitihada zozote za kuwasha generator. Cha kushangaza wanatuambia wateja twende branch ya Samora. Sijawahi kughadhibika kama leo.
Huduma hizi mbovu zitaendelea mpaka lini? Naanza kuwa na wasiwasi hata kujiuzulu kwake Mafuru. Sijui kama uongozi na bodi nzima ya NBC wanaelewa matatizo haya yanayoikabili organization yao.
Tatizo la uhaba wa wahudumu wa dirishani (tellers) nimejaribu kudadisi kwa rafiki wa karibu afanyaye kazi hapo NBC anasema ni jambo ambalo lilishaelezewa mda mwingi ila mpaka sasa halijatafutiwa ufumbuzi.
Sina hakika kama hii idara ya Operation ya hapo NBC kama inafanya kazi sawa sawa.
Nadhani ni wakati muafaka wa benki kuanza ku-outsource baadhi ya departments kuanzia hapa NBC.
Wadau mnaonaje?
 
Mtafute mkurungezi ni mtu anyesikiliza sana ushauri wa wateja wake hii ni benki yako kama umeona kasoro muone MR MAFURU ni rahisi sana kutatua hii kero.
 
Sijawahi kutembelea ofisi yeyote inayotoa huduma nikafurahia...sio nbc tu sehemu nyingi zipo hivyo...maofisini ikifika saa sita hukuti mtu..nilipata tatizo hapo tbs mtu unayemtafuta humpati eti yupo kwenye kikao...lunch...kafiwa...excuses nyingi kupita kiasi,nilikwenda duka moja wanauza simu nikaulizia bei ya iphone 5 hata kujibiwa ni kazi...wanaangalia ulivyovaa..umekuja na usafiri gani nk...ubabaishaji mtupu...customer service bado sana kwenye nchi yetu...unanunua kitu dukani mwuzaji wala haangaiki atakujibu sina change !!!!!!nenda kwenye showroom za mgari dubai hata kama huna viatu na nguo nzuri utakaribishwa kama mfalme...yatupasa kubadirika sana
 
Amtafute mafuru wapi, nyumbani kwake au? yaani huna habari kama alishaacha kazi
Mtafute mkurungezi ni mtu anyesikiliza sana ushauri wa wateja wake hii ni benki yako kama umeona kasoro muone MR MAFURU ni rahisi sana kutatua hii kero.
 
Pambaaf kabisa hawa NBC. Mkapa sijui alilogwa na nani kuiuza hii benki. Nahisi hizi ni laana za baba wa taifa.
 
Tatizo lipo kwa wateja wana uvumilivu wa ki.-----, Ingekuwa kama Huko duniani uzembe kama huo wa kutowasha Generator unapoteza 5% ya wateja mbona akili zingetengamaa, We fikiria kila siku mtu analalamikia huduma za Mtandao wa Tigo ni kero lakin bado yumo tu kama kaambiwa mtandao ni huo pekee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…