hekimatele
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 9,890
- 2,795
Wadau leo naomba niweke kero zangu nilizozikusanya over the past few months including today.
Huduma zitolewazo NBC kwa kweli si za kuridhisha hususan Corporate Branch hapo Baharini Posta. Kwanza kuna madirisha ya teller si chini ya kumi ila cha kushangaza ukiingia ndani unakuta aidha teller wawili au watatu tu ndo wanaotoa huduma kwa takriban zaidi ya watu 50 na zaidi walioko kwenye queue ambayo inaongezeka kila inaposogea dakika moja.
Ukiuliza unaambiwa wameenda lunch hususan kama umeenda mida ya mchana ila cha kushangaza unaweza kukaa zaidi ya masaa mawili kwenye queue na wasirudi huko lunch.
Leo kilichoniudhi zaidi nimefika saa 8 mchana huu hakuna umeme na hakuna jitihada zozote za kuwasha generator. Cha kushangaza wanatuambia wateja twende branch ya Samora. Sijawahi kughadhibika kama leo.
Huduma hizi mbovu zitaendelea mpaka lini? Naanza kuwa na wasiwasi hata kujiuzulu kwake Mafuru. Sijui kama uongozi na bodi nzima ya NBC wanaelewa matatizo haya yanayoikabili organization yao.
Tatizo la uhaba wa wahudumu wa dirishani (tellers) nimejaribu kudadisi kwa rafiki wa karibu afanyaye kazi hapo NBC anasema ni jambo ambalo lilishaelezewa mda mwingi ila mpaka sasa halijatafutiwa ufumbuzi.
Sina hakika kama hii idara ya Operation ya hapo NBC kama inafanya kazi sawa sawa.
Nadhani ni wakati muafaka wa benki kuanza ku-outsource baadhi ya departments kuanzia hapa NBC.
Wadau mnaonaje?