ngulyabhule
JF-Expert Member
- Apr 5, 2020
- 226
- 377
Salaam moja kwa moja kwenye mada! Wiki mbili zilizopita nilipata bahati ya mzigo kwa bei rahisi! Basi nikawa na pesa nusu ya kuulipia na nusu iliyobaki nikaona nikope hii NBC! Na kumuahidi muuzaji ndani ya siku tano tu nitamalizia nikiwa na uhakika na hii bank hasa baada ya kuamini matangazo yao lakini mpaka leo ni siku ya 11 baada ya kukamilisha taratibu zoote! Jamaa karudisha pesa na kauza kwa mtu mwingine! Na nimeenda kusitisha mkopo wanadai process zote tayari kwenye mfumo ilihali pesa yao sijaingiziwa kiniumacho nia na lengo langu lishapotezwa ni hii BANK sasa hata hiyo pesa ikija dah!