NCCR Mageuzi jipangeni upya mrudishe heshima yenu, Chadema wamewasaliti Watanzania

NCCR Mageuzi jipangeni upya mrudishe heshima yenu, Chadema wamewasaliti Watanzania

Hivi sijaelewa lengo, kwa nini hivi vyama vinapambania kuwa chama kikuu cha upinzani badala ya kuwa chama tawala? Kwa kweli Mimi bado sijaelewa halo, au lengo Ni ruzuku?
 
Nccr mageuzi kilikuwa ni chama ambacho kilisheheni wasomi na watu ambao ki msingi walijua siasa ni kitu gani.

Lyatonga Mrema, Mabere marando ,Dk S.Mvungi Masumbuko Lamwai,Dr Ringo Tenga na wengine wengi tu ambao huko mikoani walijitoa kwa ajiri ya Chama kama Mzee Cosmas Chenyenge wa Mwanza.

Upepo unanukia chama chenu sasa kinarudi katika chati hivyo mjipange ili muwe mfano bora katika kuendesha siasa za upinzani.

Hawa Chadema wamefeli kila kona maana Dj badala ya kuwa na wasomi na watu wenye akili aliwekeza kwenye kuajiri mabaunsa ambao hawana akili wala shule.

Hawajui A wala B kuhusu siasa zaidi ya ubabe na matusi.Hii ni kwa sababu Dj yoyote huwa anaamini baunsa ni bora kuliko mtu mwenye akili.

Tumieni huu muda mfupi mjipange ili Mchukue kambi ya upinzani bungeni maana Chadema imeshakufa. Na nina tumaini nchi yetu itatulia na kusonga mbele ki maendeleo.

Mbunge mmoja Leo aitwae Cosmas Mlinga ameibua kashfa mbaya sana bungeni. Kwamba Chadema huwa inawalazimisha wabunge wake kuchangia chama,wakati kinapata ruzuku.

Hata walivyopigwa virungu na magereza aliwalazimisha wachangie na akasema kama wasipochangia atawafuta uanachama.

Spika wa bunge anafahamu na alishawahi kusaidia wabunge Chadema wasinyonywe na Mbowe. Ila wenyewe mitandaoni wanajinasibu ati walichangiwa na wananchi.

Nccr mageuzi jipangeni ili muonyeshe uzalendo wa kweli.
Mkuu unajitahidi sana aise,the only thing naweza kukushauri ni kwamba,kwa kuwa wewe bado ni kijana mdogo,jitahid sana i kusoma ili uilewe nchi yetu na jinsi ccm ilivyo underdevelop this country.Kama wewe si mtoto wa familia ya Magufuli,Kikwete,mkapa,msuya,mwinyi,karume,Nyerere,Walioba,Msekwa,na familia nyingine chache hapa Tanzania,bali mihemuko yako hii inatokana na nafasi ya kuteuliwa uliyopewa,au CCM kuwa chama kilichomlea baba na mama yako, au Kama ni kwa sababu wamekuvalisha shati la kijani na suruali nyeusi basi, kusoma kutakusaidia sana huko mbeleni,Kumbuka wewe si wa kwanza na hutakuwa wa mwisho
 
Mkuu unajitahidi sana aise,the only naweza kukushauri ni kwamba,kwa kuwa wewe bado ni kijana mdogo,jitahidi kusoma ili uilewe nchi yetu na jinsi ccm underdeveloped this country.Kama wewe si mtoto wa familia ya Magufuli,Kikwete,mkapa,msuya,mwinyi,karume,Nyerere,Walioba,Msekwa,na familia nyingine chache hapa Tanzania,bali mihemuko yako hii inatokana na nafasi ya kuteuliwa uliyopewa,au CCM kuwa chama kilichomlea baba na mama Kama wanavyosema au Kama ni kwa sababu wamekuvalisha shati la kijani na suruali nyeusi basi kusoma kutakusaidia sana huku mbeleni,Kumbuka wewe si wa kwanza na hutakuwa wa mwisho
Sijakuelewa kabisa!
 
Umetandaza ukweli mtupu ,gia za angani zilinajisi mabadiliko na hiyo laana haitawaacha salama chadema;-
1) demokrasia ndani ya chama ni duni sana, toka kuteua viti maalumu na chaguzi mbali mbali, ili wenyewe mnalijua mtaacha lini? Kupanga watu kushika nafasi tofauti kwa figisu na kutishiana, na hapa ndio napomwona Lissu kakaa kimya hasemi wa hagusii, wakati naamini Lissu ni mpenda demokrasia.
2)Kuacha ajenda yao ya vita dhidi ya ufisadi, kitendo cha kupigana na ufisadi kiliijenga heshima, walitumainiwa na kweli kwetu tuliwakubali, walituchanganya pale walipo mtwaa mgombea wa urais ambae siye tuliochukizwa na ufisadi tuliona hana sifa ya chama hichi.
3) kasoro kubwa ambayo wanaendelea nayo baada ya kutambua au kutotambua kasoro zao, bado hawajitambui hivyo ni ngumu kurudi na kuuelezea umma mapungufu waliyonayo na kuelezea namna wanavyokusudia kujirekebisha ili kujenga imani kwa wanaopenda kuona upinzani imara, haya mambo ya kutishana eti sumu haionjwi, sikutegemea kutokea kwa chama chenye demokrasia,
Juu ya yote sijaona chadema wakijikosoa kuomba radhi, hata huyu Lissu anaona mengi nje ya chama, je ndani haoni bovu hata moja ambalo anaweza toka hadharani na kulipinga?
Mtazamo wangu dhidi ya kasoro ndani ya chadema;
 
lazima mpambanaji ajipe moyo!!! After all, there is "no simple dying"
Sio kujipa moyo Bali ni uhalisia kwani Kama ni kukubalika zaidi ya 90% ya Watanzania wanaikubali CHADEMA na cku jiwe akitaka kuthibitisha hili awaruhusu wafuasi wa CDM waandamane ajionee hiyo idadi
 
ni sawa na kiwete mzee kumpeleka kwenye maombi ili atembee....... ni kumtafuta lawama Mwenyezi Mungu.
 
Huna akili umeishiwa hoja. Jibu hoja acha upuuzi wa kijinga.
Hamna hoja ya kujibu hapo,naona unakazana kuleta nyuzi kwa ID tofauti tofauti!Ukiwa muandika hoja,huhitaji ID nyingi!Ila ukiwa muandika upupu watu wanakuchoka mapema,nyuzi wakiona tu jina lako wanakupuuza!Hapo ndio unaenda kufungua ID nyingine,unachokosea unarudia kuandika upuuzi na unachokwa tena!Mwisho wa siku unakuwa mtu wa ID nyingi kisa ujinga wako!
 
Back
Top Bottom