NCCR-Mageuzi v/s CHADEMA

Charuka

Member
Joined
Oct 20, 2009
Posts
56
Reaction score
18
Wakuu,
Katika pita pita yangu mitaani jana niliibukia kwenye kundi la watu wakibalizi yanayojiri ndani ya vyama vya upinzani. Mjadala ulitawaliwa na matukio ya wanachama wa CHADEMA kukimbilia NCCR. Wapenzi wa NCCR walisikika wakidokeza kuwa afterall CHADEMA ilitokana na NCCR (kamati iliyokuwa chini ya Fundikira), kwa hiyo ni vyama mtoto na mzaziwe. Mwingine akachangia kuwa ndo maana ukisoma kadi ya NCCR kwa juu kuna maneno Demokrasia na Maendeleo, ambayo Mtei aliyanakiri akaenda kuanzisha chama chake. 'Someni historia bwana'. Mjumbe mmoja alisisitiza.

Ndipo nikaondoka mahali hapo nikajaribu kupekua historia za vyama hivi. Nilijiuliza swali; kwa historia hizi, kipi chama chenye sababu kuntu ya kuanzishwa kwake, na kipi ni kwa maslahi halisi ya umma na si kundi ya watu fulani?

Hizi hapa historia zake (asomaye achunguze hata zilivyoandikwa)

Chimbuko la NCCR – Mageuzi
Wanamageuzi nchini Tanzania wamekuwa wakipigania ukombozi wa umma wa nchi yetu tangu karne ya kumi na nane. Walipinga biashara ya watumwa iliyoendeshwa na Waarabu. Waliendesha harakati dhidi ya ubeberu ukiwa katika sura ya ukoloni mkongwe kwa kupambana na wakoloni wa Kiarabu, Kijerumani na Kiingereza hadi uhuru wa Tanganyika (1961) na Zanzibar (1964) ukapatikana. Wanamageuzi wameendelea na mapambano dhidi ya ubeberu ukiwa katika sura ya ukoloni mamboleo na sura ya utandawazi, ili kuleta awamu ya pili ya ukombozi wa Mwafrika ambayo lengo lake ni ukombozi wa kiuchumi. Mwendelezo wa harakati hizi katika miaka ya 1980 ulijitokeza katika kuundwa kwa Kamati ya Taifa ya Mabadiliko ya Katiba (National Committee for Constitutional Reform) (NCCR) tarehe 12 Juni, 1991 ambayo iligeuzwa kuwa chama cha siasa tarehe 15 Februari 1992 na kusajiliwa rasmi tarehe 21 Januari, 1993 kwa jina la National Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR-Mageuzi).
Source: http://www.nccrmageuzi.or.tz/content/view/3/3/
Kuanzishwa kwa CHADEMA
Baada ya nchi ya Tanzania kutangaza rasmi kuwa nchi hii itaridhia kuanzishwa tena kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, watu wachache makini waliona vyema kutumia fursa hiyo kwa ujasiri na kuanzisha vyama vya siasa vya kushindana kisiasa na chama tawala cha CCM. Ilikuwa kazi iliyohitaji ujasiri na kujituma sana. Ingawaje serikali ilitangaza kuwa iko tayari kwa kuanzishwa kwa mfumo huo, lakini ilidhihirika wazi kuwa serikali hiyo haikuwa tayari kuupokea kwa mikono miwili. Hii ilitokana na ukweli kuwa nchi yetu ina viongozi wengi waliokulia katika utamaduni wa kutokujua kuhojiwa au kukosolewa. Hata hivyo vyama vilianzishwa na moto wa mageuzi ukaanza kuwaka kidogo kidogo.

Kutokana na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, ilibidi hata chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kusajiliwa upya. Katibu Mkuu wa CCM wakati huo akiitwa Horace Kolimba ndiye aliyekuwa Katibu Mkuu wa kwanza kuchukua hati ya usajili wa chama, na hili liliifanya CCM ijiite nambari wani kwa kuwa walichukua cheti wa kwanza na kwa kuwa walijipitishia wenyewe utaratibu kuwa CCM haikupaswa kuomba usajili kama vyama vyama vingine. Kati ya vyama vilivyoanzishwa ambavyo hadi kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 vilifikia jumla ya vyama 18 vilivyokwishasajiliwa, CHADEMA ndicho chama pekee ambacho Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alitabiri kuwa kingeweza kuiritthi CCM katika kuongoza nchi na serikali.

CHADEMA ni kifupi cha maneno
Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Chama hiki kilianzishwa kwa bidii za waasisi wake chini ya baba wa chama Mhe. Edwin Mtei. Kama ilivyokuwa kwa vyama vingine, CHADEMA kabla ya kupata usajili ililazimika kufanya kazi ngumu. Viongozi waasisi wa CHADEMA walifanya kazi ya ujasiri ambayo ilikuwa ikitafsiriwa kuwa uhaini miaka michache tu iliyopita. Walisafiri jumla ya mikoa 22 kupata wanachama ili kutimiza moja ya sharti lililokuwa la aghali zaidi katika mchakato wa usajili. Kila walipoenda walipata mwiitikio. Lakini bado watu wengi wa Tanzania walikuwa wakidanganywa na kutiwa hofu kuwa siasa ya mfumo wa vyama vingi ni chachu ya mapigano na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Source:www.chadema.or.tz/

 
National Commitee for Costitutional reform hakikuwa chama cha siasa.. Labda ungetuonyesha ni lini Chadema kilisajiliwa kama chama baada ya usajili wa NCCR - Mageuzi. Kubwa kuliko yote viongozi wote walitoka CCM sijui ndio tuseme nao walitokana na CCM au?
 
Naam, kama vile TAA ilivyoanza kivingine ikaja kugeuka chama cha siasa (TANU), unafikiri hiyo NCCR (committee) ilikuwa inajishughulisha na nini kama sio masuala ya kisiasa?
 
Naam, kama vile TAA ilivyoanza kivingine ikaja kugeuka chama cha siasa (TANU), unafikiri hiyo NCCR (committee) ilikuwa inajishughulisha na nini kama sio masuala ya kisiasa?
Nimesema NCCR hakikuwa CHAMA cha kisiasa ila ilikuwa Kamati ya Taifa ya Mabadiliko ya Katiba...
Kisha ajabu unajijibu mwenyewe kuonyesha mfano wa TAA na TANU. TAA kilipoanzishwa hakikuwa chama cha Kisiasa kilikuwa Union ya wafanyakazi wa Bandari (kama sikosei) na nyuma yake kuna historia mabyo wewe hutapenda kuisikia..
Nimemaliza mkuu asokuwa na mwana aeleke jiwe!
 
Kimsingi watu wote wa vyama wametokea CCM na wamelelewa huko. Ni jambo la kawaida mtoto akikikomaa hutafuta uhuru wake akajenga mji wake. Lakini kwa wazazi mtoto hakui. Wote wana sera zinazofanana na CCM, tofauti ni watu tu, ulaji ni uleule. Kama wamekula na kumaliza mbinu za wizi CHADEMA sio ajabu wakienda NCCR ambako labda wameona mianya ya ulaji. Ndio maana hawakwenda CCM ambao kila kiongozi ni mlaji mzuri na mahiri, ambako usipokuwa kwenye system zao utakonda tu, Hawana jipya hao. Ni sawa na muumini wa dhehebu fulani kuhamia lingine lakini kwa imani ileile ya kuamini Mungu mmoja. Tofauti yake nini? Ulaji hutofautiana mahali na mahali.

Leka
 

Kwa nini walaji hawa wasiungane ili kuwa na nguvu katika ulaji wao?
 
Heheheeeeeeeeeeeeeeeeee!
Ni ujinga kupambanisha NCCR na CHADEMA. NCCR ni chama mfu wakati CHADEMA ni chama hai.CHADEMA kina wabunge wengi na madiwani wengi lakini NCCR hawana mbunge hata mmoja bali wana madiwani wachache. Viongozi wa NCCR ni goigoi wakati viongozi wa CHADEMA ni makamanda wa vita. NCCR wanashabikia makapi kama kina Kafulila wakati CHADEMA hawashabikii makapi.
 

mkuu hapo penye nyekundu tu mkuu ndi utusaidie,unajua ni bora kusikia habari mbaya lakini ikawa ya ukweli kuliko kusikia habari nzuri afu sio ya ukweli, kwahiyo hata kama ni mbaya na hatutapenda kuisikia we iweke tu mkuu hiyo historia
 
Du!! naona Kafulila kaipandisha chati NCCR, nilishakisahau hiki chama siku nyingi!! Ila nashangaa huyu huyu Kafulila leo hii kushangilia ushindi wa Ubunge wa Kigoma kusini hata kabla ya uchaguzi kufanyika/fomu kuchapishwa!!!
 
Ni vizuri viongozi wa vyama vyaupinzani waangalie hawa watu wanaokimbia kwenye vyama vingine na kujiunga navyama vyao kwani yawezekana wengine wametumwa ili kufifisha nguvu ya chama, au pia wengine wanamatatizo ya kudumu, nawatakapo wakaribisha, basi wajue wanawakaribisha na hayo matatizo waliyo nayo na mwisho ni kuvurugana tu.
 
Ulimbo mtizamo wako ni sahihi kabisa. Hawa watu hawana sera na hawajui wanataka kuifanyia nchi kitu gani. Matatizo yao makubwa ni kutotaka kutofautiana na mtu yeyote. Analofikiri yeye ndilo sahihi na ukimkosoa wewe ni adui.

Halafu umbea umbea wa kusemana ndani ya chama. Watu wanaochukulia masuala ya chama kuwa personal hawatakiwi kwenye uongozi wa ngazi yoyote kwani lazima wataleta mfarakano.
 
kaka kama hujui nyamaza.sio NATIONAL COMMITEE FOR CONSTITUTION ni National convention for construction reform.Naona mapenzi na ushabiki vinapofua bongo za watanzania.
Go to work..Tanzania needs you,dont spend big portion of your time browsing
 
Du!! naona Kafulila kaipandisha chati NCCR, nilishakisahau hiki chama siku nyingi!! Ila nashangaa huyu huyu Kafulila leo hii kushangilia ushindi wa Ubunge wa Kigoma kusini hata kabla ya uchaguzi kufanyika/fomu kuchapishwa!!!

Mkuu namwonea huruma huyu dogo, nafikri hajui kusoma alama za nyakati na hajastukia siasa za inji hii zinavyoenda.

Kule kigoma ammulize Dr Kaburu atamsimulia vizuri - Tunamkaribisha kwa miguu miwili na tiketi yake yake ya NSSR
 
kaka kama hujui nyamaza.sio NATIONAL COMMITEE FOR CONSTITUTION ni National convention for construction reform.Naona mapenzi na ushabiki vinapofua bongo za watanzania.
Go to work..Tanzania needs you,dont spend big portion of your time browsing
Notradammus,
Unapenda kukosoa kumbe wewe ndo mambo yamekupita kushoto. NCCR iliundwa mnamo mwaka 1991, kabla ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini. Wakati huo ilikuwa ikijiita Kamati ya Kitaifa ya kudai mabadiliko ya kikatiba (hususan kutoka katika mfumo wa chama kimoja ili Tanzania iwe na mfumo wa vyama vingi) kwa kiingereza iliitwa National Committee for Constitutional Reform. Vyama vingi viliporuhusiwa na utawala wa mzee Ruksa, kamati hii ikajibadilisha kuwa chama cha siasa, kifupisho kikabaki kile kile (NCCR) lakini zile CC yakawa maneno tofauti, badala ya committee wakatumia convention, na badala ya constitution wakatumia Construction.
Marehemu Chifu Fundikira, aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati, alitoka akaunda chama chake (UMD), Katibu Mkuu wa kamati (Wakili Marando) akachukua uenyekiti wa kwanza wa chama. CCM ilipomtema Mrema, Marando akakabidhi uenyekiti kwa Mrema, kama vile kubadilishana shati. Mrema alipolikoroga akakimbilia TLP, uenyekiti ukachukuliwa na Marehemu Aidari Magutto, walipofanya uchaguzi baadaye Mbatia akaukwaa uenyekiti. Mwaka jana alipambana na Bura Dodo, ambaye hata hivyo aliingia mitini, hivyo Mbatia ni M/kiti hadi leo.
 

Mfu huyu kiboko! wanaojigamba wako hai wanaliona jinamizi lake, he he he!
 


Si kweli kwamba watu wote wa Vyama wametokana na CCM . Elezea kwa undani una maana gani .Si kila mtanzania aliyeko kwenye Siasa za upande wa pili basi amekuwa mwana CCM . Think again
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…