Wakuu,
Katika pita pita yangu mitaani jana niliibukia kwenye kundi la watu wakibalizi yanayojiri ndani ya vyama vya upinzani. Mjadala ulitawaliwa na matukio ya wanachama wa CHADEMA kukimbilia NCCR. Wapenzi wa NCCR walisikika wakidokeza kuwa afterall CHADEMA ilitokana na NCCR (kamati iliyokuwa chini ya Fundikira), kwa hiyo ni vyama mtoto na mzaziwe. Mwingine akachangia kuwa ndo maana ukisoma kadi ya NCCR kwa juu kuna maneno Demokrasia na Maendeleo, ambayo Mtei aliyanakiri akaenda kuanzisha chama chake. 'Someni historia bwana'. Mjumbe mmoja alisisitiza.
Ndipo nikaondoka mahali hapo nikajaribu kupekua historia za vyama hivi. Nilijiuliza swali; kwa historia hizi, kipi chama chenye sababu kuntu ya kuanzishwa kwake, na kipi ni kwa maslahi halisi ya umma na si kundi ya watu fulani?
Hizi hapa historia zake (asomaye achunguze hata zilivyoandikwa)
Chimbuko la NCCR Mageuzi
Wanamageuzi nchini Tanzania wamekuwa wakipigania ukombozi wa umma wa nchi yetu tangu karne ya kumi na nane. Walipinga biashara ya watumwa iliyoendeshwa na Waarabu. Waliendesha harakati dhidi ya ubeberu ukiwa katika sura ya ukoloni mkongwe kwa kupambana na wakoloni wa Kiarabu, Kijerumani na Kiingereza hadi uhuru wa Tanganyika (1961) na Zanzibar (1964) ukapatikana. Wanamageuzi wameendelea na mapambano dhidi ya ubeberu ukiwa katika sura ya ukoloni mamboleo na sura ya utandawazi, ili kuleta awamu ya pili ya ukombozi wa Mwafrika ambayo lengo lake ni ukombozi wa kiuchumi. Mwendelezo wa harakati hizi katika miaka ya 1980 ulijitokeza katika kuundwa kwa Kamati ya Taifa ya Mabadiliko ya Katiba (National Committee for Constitutional Reform) (NCCR) tarehe 12 Juni, 1991 ambayo iligeuzwa kuwa chama cha siasa tarehe 15 Februari 1992 na kusajiliwa rasmi tarehe 21 Januari, 1993 kwa jina la National Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR-Mageuzi).
Source: http://www.nccrmageuzi.or.tz/content/view/3/3/
Kuanzishwa kwa CHADEMA
Baada ya nchi ya Tanzania kutangaza rasmi kuwa nchi hii itaridhia kuanzishwa tena kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, watu wachache makini waliona vyema kutumia fursa hiyo kwa ujasiri na kuanzisha vyama vya siasa vya kushindana kisiasa na chama tawala cha CCM. Ilikuwa kazi iliyohitaji ujasiri na kujituma sana. Ingawaje serikali ilitangaza kuwa iko tayari kwa kuanzishwa kwa mfumo huo, lakini ilidhihirika wazi kuwa serikali hiyo haikuwa tayari kuupokea kwa mikono miwili. Hii ilitokana na ukweli kuwa nchi yetu ina viongozi wengi waliokulia katika utamaduni wa kutokujua kuhojiwa au kukosolewa. Hata hivyo vyama vilianzishwa na moto wa mageuzi ukaanza kuwaka kidogo kidogo.
Kutokana na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, ilibidi hata chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kusajiliwa upya. Katibu Mkuu wa CCM wakati huo akiitwa Horace Kolimba ndiye aliyekuwa Katibu Mkuu wa kwanza kuchukua hati ya usajili wa chama, na hili liliifanya CCM ijiite nambari wani kwa kuwa walichukua cheti wa kwanza na kwa kuwa walijipitishia wenyewe utaratibu kuwa CCM haikupaswa kuomba usajili kama vyama vyama vingine. Kati ya vyama vilivyoanzishwa ambavyo hadi kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 vilifikia jumla ya vyama 18 vilivyokwishasajiliwa, CHADEMA ndicho chama pekee ambacho Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alitabiri kuwa kingeweza kuiritthi CCM katika kuongoza nchi na serikali.
CHADEMA ni kifupi cha maneno Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Chama hiki kilianzishwa kwa bidii za waasisi wake chini ya baba wa chama Mhe. Edwin Mtei. Kama ilivyokuwa kwa vyama vingine, CHADEMA kabla ya kupata usajili ililazimika kufanya kazi ngumu. Viongozi waasisi wa CHADEMA walifanya kazi ya ujasiri ambayo ilikuwa ikitafsiriwa kuwa uhaini miaka michache tu iliyopita. Walisafiri jumla ya mikoa 22 kupata wanachama ili kutimiza moja ya sharti lililokuwa la aghali zaidi katika mchakato wa usajili. Kila walipoenda walipata mwiitikio. Lakini bado watu wengi wa Tanzania walikuwa wakidanganywa na kutiwa hofu kuwa siasa ya mfumo wa vyama vingi ni chachu ya mapigano na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Source:www.chadema.or.tz/