the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Wakuu NCCR nao nao wanadai hawapo kuunganisha nguvu na chama chochote cha upinzani, wanasahau kidole kimoja hakivunji chawa
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
=====
Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema hakitajiunga na chama chochote cha upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mwenyekiti wa chama hicho, Ambar Khamis, ametoa kauli hiyo leo, Februari 18, 2025, katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Ilala, jijini Dar es Salaam.
"Sisi NCCR tutakuwa peke yetu, hatutakuwa na muungano na vyama vingine kutokana na madhara tuliyoyapata mwaka 2015 baada ya kujiunga na UKAWA. Tulipata wabunge wanne katika majimbo mbalimbali, lakini tukabaki na mbunge mmoja pekee, hali iliyotufanya kupoteza majimbo yetu," alisema Khamis.
Ameongeza kuwa kulikuwepo na makubaliano ndani ya muungano huo, lakini baadhi ya vyama wenza vilishindwa kuyatekeleza.
Aidha, Khamis amesema kuwa NCCR-Mageuzi tayari imeanza vikao vya Kamati Kuu kwa ajili ya maandalizi ya chaguzi za ndani ya chama.
"Vyama vingine kama ACT-Wazalendo, CAF, na CHADEMA vimeshafanya chaguzi zao, sasa ni zamu yetu," alisema.
Amebainisha kuwa chama hicho kinatarajia kufanya mkutano mkuu wa ngazi za kitaifa, mikoa, na wilaya mwezi Aprili mwaka huu, ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.