Nchi 10 za Afrika zenye huduma bora za Polisi, Tanzania haipo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Ripoti ya Afrobarometer iliyochapishwa hivi karibuni, imebaini kuwa huduma za polisi barani Afrika zinakabiliwa na changamoto kubwa za uadilifu na weledi, huku asilimia ndogo ya raia wakiridhika na utendaji wa vyombo hivyo vya usalama.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyokusanya maoni ya raia kati ya mwaka 2021 na 2023, ni mmoja tu kati ya Waafrika watatu anayesema anaridhishwa na utendaji wa polisi.

Kwenye list hii hakuna nchi yoyote ya Afrika Mashariki, tazama;

1. Botswana
2. Afrika Kusini
3. Benin
4. Tunisia
5. Senegal
6. Sao Tome na Principe
7. Seychelles
8. Ghana
9. Cape Verde
10. Lesotho

Chanzo: Business Insider Afrika
 
Tanzania ipo kwenye huduma nzuri za uganga wa kienyeji na imani za kishirikina.
 
EA?
 
Ningeshangaa kama Tanzania ingekuwepo.
 
SA hapana nakataa
 
tz tuna police force sio police service
 
Botswana πŸ‡§πŸ‡Ό hiyoo nchi wanaishi kama. Wapo peponi hawana mamboo mengi aseee Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ njaaa polisi anakupa kesi anataka tuu pesa yaan polisi na raia ni maadui kabisaaa
Polisi bongo wakijuwa una mpunga lazima waje wakutemeshe

Ova
 
Nawapongeza Kenya, Uganda, Rwanda na Zambia, zimbabwe na Egypt kwa kuwemo kwenye list
 
Hawa wazeewa nongwa na mlungula, hawawezi kuwa watu wa maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…