Nchi 54 duniani zinaruhusu wasichana kuolewa mapema kwa kati ya miaka 1-3 kuliko wavulana

Nchi 54 duniani zinaruhusu wasichana kuolewa mapema kwa kati ya miaka 1-3 kuliko wavulana

Zawadi Mkweru

Member
Joined
Jan 11, 2017
Posts
5
Reaction score
19
Ndoa za utotoni mara nyingi hutokea kati ya msichana mdogo na mwanaume mzee. (Mfano miaka 15 kwa miaka 75) Msichana ananyimwa haki yake ya kuchagua mwenzi na kupewa uwezo mdogo nyumbani na hata kunyanyaswa.

Kwa mujibu wa Shirika la watoto duniani (UNICEF), karibu nusu (45%) ya wanawake wote wenye umri wa miaka 20-24 waliripotiwa kuolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Karibu msichana mmoja kati ya wasichana watano (17%) huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 15.

India ina idadi kubwa zaidi ya biharusi ulimwenguni - theluthi moja ya jumla ya wote ulimwenguni. Bangladesh ina kiwango cha juu zaidi cha ndoa za utotoni katika Barani Asia (kiwango cha nne cha juu zaidi ulimwenguni). Nepal pia ina viwango vya juu zaidi vya ndoa za utotoni Barani Asia kwa wavulana na wasichana.

Kwa mujibu wa mtandao wa girlsnotbirdes.org, kila mwaka wasichana milioni 12 huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18. Hiyo inamaanisha ni wasichana 23 huolewa kila dakika - kuolewa kwao mapema hufanya maendeleo yao ya kibinafsi na ustawi kuwekwa hatarini.

Ulimwenguni kote, wasichana ambao huolewa kabla ya kufikisha miaka 15 wana uwezekano mkubwa wa kukumbwa na unyanyasaji wa kingono kutoka kwa wenzia wao. Asilimia 50 ya wasichana walioolewa kabla ya kufikisha miaka 15-19 kutoka nchini Bangladesh, Tanzania, Uganda na Zimbabwe, wamekumbana na unyanyasaji kutoka kwa waume zao au wenzi wao.

Utafiti wa 2017 wa Child Marriage Youth Friendly ulibaini ndoa za utotoni zinatokea sana katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Dodoma na Mara nchini Tanzania. Katika mikoa hiyo zaidi ya 50% ya wasichana waliolewa kabla hawajafikia umri wa miaka 18.

Katika mkoa wa Iringa, msichana 1 kati ya 10 ameshaolewa kabla hajafika umri wa miaka 18 na msichana mmoja kati ya watano wa Dar es Salaam ameshaolewa.

Kwa mujibu wa takwimu za UNICEF za kati ya mwaka 2010 na 2017, Tanzania ni ya tatu kwa kuwa na viwango vya juu vya ndoa za utotoni baada ya Sudan Kusini na Uganda.

Sudan Kusini kiwango cha watoto wa chini ya miaka 18 wanaoozwa ni asilimia 52 na nchini Uganda ni asilimia 40. Tanzania ni asilimia 31. Nchini Kenya, ni watoto asilimia 23 wanaoozwa kabla ya kutimiza miaka 18.

Ndoa za utotoni hutokea zaidi kwenye maeneo ya vijijini ambako umaskini umeenea zaidi, elimu ya sekondari haipatikani kwa urahisi na hakuna elimu nyingi kuhusu afya ya uzazi (uzazi wa mpango) ukilinganisha na maeneo ya mijini.

Watoto walioolewa katika umri mdogo wana uwezekano mkubwa wa kuamini kuwa mwanaume ana haki ya kumpiga mkewe. Ulimwenguni kote, asilimia 44 (girlsnotbrides.org) ya wasichana wenye umri wa miaka 15-19 wanafikiria mume au mwenzi ana haki ya kumpiga mkewe au mwenzi wake.

Ndoa za utotoni ni ukiukwaji wa haki za binadamu ambao ni lazima tuumalize ili kufikia mustakabali bora kwa watu wote.

Wasichana wanaoolewa mapema huwa hawajakua wala kuwa na utayari wa kuwa wake wala mama. Hukumbana na changamoto nyingi ikiwemo matatizo wakati wa ujauzito na hata wakati wa kujifungua, maambukizi ya UKIMWI na unyanyasaji wa kijinsia majumbani

Ndoa za utotoni zinakiuka haki za mtoto wa kike ikiwemo Afya, Elimu na kupata fursa. Ndoa hizi huwatengenezea wasichana mazingira ya kunyanyasika kijinsia katika maisha yao yote na kuwafunga katika mazingira ya umaskini. Kutokana na upatikanaji mdogo wa elimu na fursa za kiuchumi, wao pamoja na familia zao wana uwezekano mkubwa wa kuishi katika umasikini kwa muda mrefu.

Kutengeneza ulimwengu usio na dhuluma kwa wanawake na wasichana - inamaanisha sisi sote, kuchukua hatua za pamoja leo na kila siku. Kuanza kwa kutambua changamoto zilizopo na kuwasikiliza wanawake, kuzungumza yanayotokea, kupinga utani na tabia ambazo hazikubaliki, sote tuna jukumu la kufanya katika hili.

Kuongezeka kwa 10% ya nguvu katika Kukomesha ndoa za utotoni kutapunguza unyanyasaji kutoka kwa wenzi hawa kwa zaidi ya 10% nchini Ethiopia, Msumbiji, Nigeria na Uganda.
 
Back
Top Bottom