Nchi 8 zenye sheria zinazoshangaza

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Huu ni ulimwengu wa kanuni, taratibu
na sheria ambazo kufuatwa ni wajibu wa kila mtu ingawa zipo kanuni, taratibu na sheria nyingine zinaajabisha sana na ninazo hapa sheria 8 kwenye sehemu mbalimbali za dunia.


1: Polisi kukamata wenye UKIMWI – Ugiriki

Nchini Ugiriki Polisi wanaruhusiwa kumkamata Mtu yeyote anayeshukiwa kuwa na HIV… Polisi pia wanaruhusiwa kulazimisha watu kupima HIV , kutangaza majina ya wenye HIV hadharani na kuwafungia majumbani mwao.


2: Ruhusa ya kumpiga mkeo – Kansas

Katika mji wa Arkansas, Marekani bado kuna sheria ambayo ilianzishwa miaka ya 1800 ambayo inamruhusu mume kumpiga mkewe lakini mara moja kwa mwezi.


3: Mwenye mustachi haruhusiwi kubusu – Iowa

Kuwa na mustachi au hata ndevu sio tatizo katika sehemu nyingi duniani lakini katika mji wa Iowa Marekani ni kama vile unaambiwa usiwe na mustachi kiaina baada ya watu wenye mustachi kukatazwa kumbusu mwanamke hadharani.


4: Tangazo la ndoa kwenye gazeti – Ugiriki

Nchini Ugiriki kama unataka kuoa, sheria inawataka wenye nia ya kufanya hivyo kuchapisha tangazo la ndoa kwenye gazeti (kwa kigiriki) au kwenye ubao wa matangazo.


5: Mke kumuua Mumewe msaliti – Hong Kong

Hong Kong kuna sheria ambayo inaruhusu Mke kumuua Mumewe kama atabaini anamsaliti ambapo hata hivyo anatakiwa kumuua kwa mikono yake pasipo kutumia silaha yoyote.


6: Kusahau Birthday ya mkeo – Samoa

Ni wangapi huwa na kumbukumbu nzuri ya siku ambayo wamezaliwa watu wao wa karibu hasa Mke/Mume? Unaambiwa kwenye nchi ya Samoa ni kosa kwa mume kusahau birthday ya mkewe.


7: Matembezi na Mbwa – Turin, Italia

Baadhi ya sehemu ni jambo lisilo la kawaida mtu kutembea na mbwa katika matembezi ya kawaida lakini hilo ni tofauti katika mji wa Turin, Italia ambapo wamiliki wa Mbwa wanatakiwa kutembea na Mbwa wao angalau mara tatu kwa siku.


8: Kuibia mitihani – Bangladesh

Hakuna nchi inayoruhusu Wanafunzi wake waibie majibu wakati wa mitihani, unaambiwa Bangladeshi imeweka sheria kuwa watoto wa miaka 15 na watu wazima, wanaweza kufungwa kama watakutwa na kosa la kuibia kwenye mitihani yao ya mwisho.
 
WAKOREA WAAGIZWA KUNYOA KIDUKU KAMA RAISI WAO KIM


Wanaume Korea Kaskazini wanakabiliwa na mtihani mpya katika taifa lao; wa kunyoa nywele kwa mtindo ulioamuliwa na rais wao.

Watake, wasitake kuanzia sasa kila mwanamume atalazimika kunyoa nywele zake kwa mtindo anaoupenda Rais Kim Jong- un.

Kiongozi huyo kijana, aliyerithi wadhifa huo baada ya kifo cha baba yake, hana mzaha hasa kutokana na nia yake ya kujenga mfumo mpya wa utawala ambao matakwa yake tu ndiyo ya kufuatwa.

Ni wiki mbili sasa tangu serikali ya nchi hiyo kutoa agizo linalowataka wanaume kunyoa kama rais wao, huku wanawake nao wakielekezwa kutengeneza nywele zao kwa aina 18 tofauti na si zaidi ya hapo.

Hilo ni moja ya maagizo yenye utata kuwahi kutolewa chini ya utawala wake, ambapo amekuwa akifanya jitihada za kujijengea mizizi, ikiwamo kuwaondoa na kuwaadhibu wale waliokuwa katika utawala wa baba yake wanaoonekana kutokubaliana na aina yake ya uongozi.

WAKOREA WAAGIZWA KUNYOA KIDUKU KAMA RAISI WAO KIM ~ BONGO POST
 
Tanzania inaongoza kwa Matendo mazuri. Km kuondoa watu wote kazini ambao hawajafika form iv.na wanasiasa qawe la saba tena wajue tuu kusoma na kuandika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…