Nchi ambayo haijapata chanjo ya Corona inaweza kutengwa?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,650
Reaction score
21,014
Iko hivi wakuu. Virusi vikipata mazingira mazuri huwa vinabadilika kila leo. Kubadilika huko kunaweza toa kirusi kikali kisichosikia dawa wala chanjo.

Hizi chanjo zimetengenezwa kuzuia kirusi kwa namna kiliyopo sasa. Kinaweza kubadilika na kufanya chanjo hiyo isifanye kazi au ikafanya kwa ufanisi mdogo sana.

Sasa watu wasio kuwa na chanjo ni mazalia ya virusi hivi na ni kiwanda cha virusi kubadilika na kutoa aina mpya. Naona kuwa watu hawa watazuiwa kwenda nchi nyingine kwa sababu wanaweza wapelekea wengine strains ambazo hazisikii dawa. Pia watu hata waliopata chanjo wataogopa kutembelea nchi hizi kwa sababu ya kuogopa kukumbana na strains kali za virusi.

Nyinyi mnaonaje, kuna uwezekano wa nchi ambazo hazijapata chanjo au kuna coverage ndogo ya chanjo kutengwa?
 
Wakati ukifika ndio tutajua, ni swala la muda tu lakini kama chanjo wakichomwa wao wanaogopa nn sasa maana itakuwa haina ubora bado hata kama virusi wanajibadilisha badilisha lkn kirusi kinaendelea kubaki ni kile kile.
 
Sio kwamba waliochanjwa wanageuka mazombi
Wageuke mazombi kwa sababu gani? Mbona watoto wachanga hadi leo hii wanachomwa chanjo ya polio na hawabadiliki kuwa mazombi? Watanzania waliochomwa chanjo nyingine maarufu kama vile chanjo ya ndui walibadilika kuwa mazombi?

Wewe chanjo ulizowahi kuchomwa zimekubadilisha kuwa Zombi? Wewe ni Zombi sasa hivi kutokana na chanjo kadhaa ulizowahi kuchomwa? Unaongea kama mtoto mdogo alievaa pampas!
 
Tanzania inakuja kuwa world COVID-19 virus center for mutations!
nasubili wale waliochanjwa after 5 years tutaanza kuona vibwanga.kama wengine waliochanjwa wamekata kamba,wengine wako hoi vitandani.sasa wale ambao wali sustain na reaction ya chanjo,naamini baadae tutaanza kuona matokeo.yajayo yatafurahisha.time will speak.
 
Hivyo vimbwanga vitasababishwa na nini?Mbona watoto wachanga hadi leo hii wanachomwa chanjo ya polio na hatuoni vimbwanga?Watanzania waliochomwa chanjo nyingine maarufu kama vile chanjo ya ndui walionyesha vimbwanga?Wewe chanjo ulizowahi kuchomwa kadhaa ulisababisha vimbwanga?
 
Wakazi wa dunia wanakwenda kujaa matundu miilini mwao kwa sababu ya misindano ya chanjo
 
Uko sahihi kabisa! [emoji122][emoji122]
 
Uko sahihi, mfano mzuri ni kirusi cha SA, kimekuwa hatari zaidi. Naogopa isije kuwa Chunya ndio variant nyingine.
 
Watengeneza chanjo za Korona hawana tofauti na wanaobet, yaani wanafanya trial and errors mpaka kwenye afya za watu.

Ukiangalia hivi virusi vya kutoka Brazil, South na UK vimeanza wakati wa watu wameanza kupewa hizi Chanjo na hivi virusi vipya vinasambaa kwa kasi na ni vikali kuliko vya kwanza.

Saa nyingine bora kusubiri, kijifanya kimbelembele unaweza ukatibua kinga ya mwili wako, ukawa rahisi kupata maambukizi.
 
akili ndogo tu inatosha kukupa jibu.polio inachanjo moja,hiyo ndui inachanjo moja,lakini pia utafiti ulifanyika kwa muda mrefu wa hizo chanjo ndio maana wakakubaliana baada ya kujieidhisha kwa kina juu ya ufanisi wa hizo chanjo,hawakuwa na haja ya kuja na lundo la chanjo kwa case moja. CHANJO NI KIRUSI AMBACHO KINAFENGENEZWA KU FIGHT KIRUSI HASIMU MWILINI,sasa ukikitengeneza kwa kubahatisha lazima kitakufurahisha tu...Corona ni ugonjwa wa corony aina moja ya virus ,hivyo Ni case moja why wanakuja na lundo la chanjo kwa case moja???? jibu hawana uhakika na chanjo ipi itatoa majibu positive.... Concluding;bado wapo kwenye trial and error.
Quation....kwenye trial and error tegemea madhara makubwa kwa sababu upo kujaribu kupata suluhisho.
Over
 
Hizo chanjo ulizo orodhesha hapo, wenda ndio chanzo cha mfumuko wa mashoga duniani.

Kipindi nikiwa makuzi (dogo janja) miaka ya tisini kushuka chini, mashoga walikua wakuwatafuta kwa tochi, tofauti na hivi sasa, kila mtaa kuna ***** wake.

Napinga chanjo kwa nguvu zote.
 
Unauliza kwa nini wamekuja na chanjo nyingi kwani hapa duniani nchi ikiamua kutengeneza chanjo yake ili kuendeleza taaluma yake katika tafiti za dawa ni kosa?Kwani hata Tanzania si inaweza kutengeneza chanjo yake?Mfano kungekuwa na chanjo moja tu ya marekani peke yake halafu Tanzania nao wakatengeneza chanjo yao ili kukuza taaluma yake katika mambo ya madawa ya binadamu still ungeuliza ni kwa nini dunia imetengeneza chanjo zaidi moja?
 
Wewe tayari ulishachanjwa chanjo ya polio pamoja na chanjo nyingine ulivyokuwa mdogo,ina maana wewe sasa hivi ni shoga pia?
 
Ila wadanyika kwa porojo mko vzr....hivi nyinyi chanjo yenu mliyogundua iko wapi

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Ila wadanyika kwa porojo mko vzr....hivi nyinyi chanjo yenu mliyogundua iko wapi

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Tatizo sio chanjo yetu bali uhakika wa chanjo yenyewe ,ndio hatuna uwezo wa kutengeneza chanjo,lkn sio kigezo wa kukubali,kila chanjo bila kujilizisha.

Alafu hajakatazwa mtu kupata chanjo,kuna mzigo wa chanjo unafika hapo Kenya,wewe mwenye hofu ya Corona nenda kachanjwe hujakatazwa kwani afya yako na mwili ni wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…