Nchi ambayo haijapata chanjo ya Corona inaweza kutengwa?

Chanjo hazifanyi kazi hivyo. Yaani kirusi kikapambane na kirusi!.
kuna njia nyingi ya kutengeneza chanjo. Njia ya kwanza ni kutumia kirusi kilichokufa. Mfano, wanachukua kirusi cha korona kilichokufa na kumchoma mtu. Kinga ya mtu itaona kuna kitu kigeni, itapambana nacho. Siku ikikutana na kirusi hai inakuwa imejua jinsi ya kupambana nacho.

Njia nyingine ni kutumia kirusi kilichopunguzwa nguvu, mfano unapunguza nguvu kirusi cha korona na kumchoma mtu, kinga itapambana nacho, siku ikikutana na chenyewe inakuwa inajua nini cha kufanya.

Aina ya tatu ni kuchukua sehemu ya kirusi, mfano unaweza kuchukua ile miiba ya kirusi cha korona na kumchoma mtu. Kinga ya mwili ikireact inakuwa imeshajifunza namna ya kupambana na kirusi cha korona. Zipo njia nyingi na ndiyo sababu kuna kinga nyingi.
Hata hizi kinga tunazochomwa zipo za aina nyingi. Ukijua jinsi kinga inavyofanya kazi hakuna haja ya kuogopa.
 
Hivi huwa mnadanganya kwa maslahi ya nani? kama watu hawajachanja ndo wanakuwa more susceptible to infection, hivyo virusi havitumii jitihada kubwa kuambukiza na kuzaliana. Virusi wata-mutate iwapo watakutana na upinzani, mfano kinga iliyotokana na chanjo au kinga iliyotokana na mtu kuambukizwa na kupona au kama dawa (antiviral drugs) zitatumika kutibu.....sasa unavotuambia kwamba chanjo haziwezi ku-drive mutations tunakuwa hatukuelewi. Siyo lazima kila mtu aandike mambo ya kitaalamu ambayo hajasomea ili mradi aonekane na yeye kaleta uzi....
 
Kama utakuwa umechanjwa maana yake utakuwa na kinga na virus haviwezi kuzaliana ndani yako. Na kama havizaliani basi haviwezi kumutate. Uksipochanjwa au msipochanjwa maana yake virus vitakuwa vinazaliana kwa fujo. Hapo mtakuwa shamba la mutation.
 
Kama utakuwa umechanjwa maana yake utakuwa na kinga na virus haviwezi kuzaliana ndani yako. Na kama havizaliani basi haviwezi kumutate. Uksipochanjwa au msipochanjwa maana yake virus vitakuwa vinazaliana kwa fujo. Hapo mtakuwa shamba la mutation.
Nani aliyekwambia hizo mnazoita chanjo zinazuia virusi kuambukiza na kuzaliana, vipi kama asilimia kubwa ya watu walishaambukizwa wakapata herd immunity. Msijaribu kumeza kila kitu ambacho wazungu wanajaribu kuwaaminisha, jaribu kutumia akili yako au kuongeza uelewa wako wa mambo na reasoning.
 
Kusema watu wajenge herd immunity maana yake wale wote ambao wako vulnerable Wafe. Herd immunity ndiyo inajengwa hivyo kifupi ni survival of the fittest. Unataka hivyo? Kwanza unafikiri inachukua muda gani kujenga hiyo kitu, ndui ingechukua muda gani?

Virusi vinazaliana ndani ya host/ binadamu sasa kutumia chanjo ni kama kuharibu mazalio ya virusi.
 
Hizo wanazoita chanjo hazitoi life-long immunity kama hiyo ndui unayosema, which means utahitaji booster kila baada ya miezi 6, hiyo ni biashara nzuri sana kwa watengezaji wa hiyo chanjo, on the other hand huwezi kutumia kila bindamu duniani kama panya wa majaribio kwa chanjo ambayo bado ipo kwenye utafiti, na mbaya zaidi hayo makampuni ya chanjo hawajabeba uwajibikaji wowote kwa vifo au madhara ya muda mfupi na muda mrefu yatakayosababishwa na hiyo chanjo ya majaribio, maana kila mtu ni kama analazimishwa kudungwa hiyo chanjo bila ridhaa wala kulipwa chochote kwa kushiriki kwenye majaribio ya chanjo.
 
Imenisikitisha hapo kwenye makampuni hayajabeba uwajibikaji yaani maana yake,
Madhara yeyote yale yatakayo kupata si juu yako.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Unaijua polio? Jiulize bila chanjo ingekuaje
 
Tena Pampas ilojaa mkojo hahahahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…