Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Hii si nchi ya kusadikika uliyoisoma kwenye kitabu cha Hayati Shaban Robert, wala si nchi ya Wagagagigikoko na Mfalme wake Huihui dikiteta aliyepigwa na mgeni Bulicheka na akapoteza ufalme.
Hii ni nchi inayopatikana Afrika mashariki, kusini mwa jangwa la Sahara. Ni Muungano wa Tanganyika Huru na visiwa vya Zanzibar na Pemba.
Ni ndani ya Utawala mpya (sijasema uongozi) kunapatikana dhana na falsafa mpya ambapo viongozi wa serikali na Chama kinachounda serikali kinafurahia vitendo vya mateso Kwa raia wake. Nitatoa mifano michache ya furaha na vicheko vya viongozi wa serikali Kwa mateso ya raia;
1.Mateso Kwa Wamasai Ngorongoro yanayofanywa na Askari wa TANAPA na Sasa Polisi yanafurahiwa vilivyo na viongozi wa Chama na serikali Kwa Kisingizio cha uwekezaji. Huko uchumi umekuwa muhimu kuliko uhai wa watu.
2.Mauaji na mateso Kwa wanasiasa wa upinzani yanafurahiwa Kwa kicheko kikubwa na Chama na serikali yake. Mfano ni uonevu waliofanyiwa viongozi wa CHADEMA wakiwa Mbeya, kamishna wa Polisi aitwaye Awadh Haji Kwa Sasa anatembea Tanzania nzima akihimiza Askari wake wasisikilize kauli za wanasiasa Bali waendeleze Moto wa mateso Kwa Kila anayekosoa serikali. Viongozi wa serikali Kwa furaha kabisa wanamuona Awadhi jembe Kwa majeraha na mateso anayowapa Wapinzani.
3.Utekaji na upotezaji wanaharakati unafurahiwa pakubwa na viongozi wa serikali na Chama Kwa vile Una lengo la kupunguza ukosoaji.
4.Matukio ya udhalilishaji na ubakaji yanayofanywa na watumishi wa serikali yanafurahiwa na kufubazwa na viongozi wa Chama na serikali ili kulinda image ya chama na serikali. Mfano mzuri ni tukio la Babati lililomhusu Mbunge Gekul na la binti ya Yombo Dovia linalomgusa "Afande" kama msukaji wa tukio.
Hayo ni mqchache Kati ya mengi ambayo badala ya huzuni yanaipa furaha serikali na kukifariji Chama tawala Kwamba kiko salama kwenye mikono ya vyombo katili vya Dola.
Pema usijapopema ukipema si pema tena.