Nchi hii haiwezi endelea kama tusipokubali kufikia hatua hii ya Kujikana

Nchi hii haiwezi endelea kama tusipokubali kufikia hatua hii ya Kujikana

Gobole Lenye Risasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
11,519
Reaction score
23,693
Kwa sasa utagundua hakuna kitu kinachotuunganisha watanzania. Hakuna.

Unaweza sema ni chama. chukulia ccm.utagundua wakati wa mapambano kati ya ccm na cdm ccm wote watakuwa dhidi ya cdm.watawatenga ccm wakiamini wao wameshikamana.

Ila ingia ndani ya ccm.waweke kwenye udini.watajigundua wote ni ccm lakini wana dini tofauti.kuna waislamu,wakristo na wadini za kienyeji. watatengana kwa style hiyo hivyo watamkataa yule na kumkumbatia huyu kwa misingi hiyo hiyo.

Wakikaa katika kivuli cha dini moja watakuja baguana kwa madhehebu yao. Wakikaa katika madhehebu watakuja baguana kwa ukabila.watagundua kwenye ukabila kuna koo n.k

Hivyo kwa asilimia kubwa kuna dhambi ya ubaguzi kwa kila ngazi ambao unatuondolea uzalendo kwa taifa hili. Hatuwezi fikia kuwa na jambo la pamoja kwa kuwa kuna watu wanafaidika na ubaguzi huu kwa kiasi kikubwa.

Kama tufikie hatua tuseme sisi ni watanzania na tunaangalia maslahi ya Tanzania na watu wake. Kwa ajili yetu na kizazi chetu. Nchi hii itaendelea kwa kasi kubwa sana kama China n.k
 
Back
Top Bottom