Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Hata mtu kipofu anaona kabisa Tanzania imebadilika na inazidi kubadilika kuelekea kubaya zaidi siku hadi siku. Muungano unazidi kuporomoka kukiwa na viashiria vinavyokua vya u-Bara - na U-Zanzibar
Wazanzibar waneanza kuwachukia Watanganyika na Watanganyika kuwachukia Wa Zanzibar
Udini unazidi kukua kukiwa na hisia kwamba Wakristo wanataka kuondoa uongozi wa Kiislamu na Waislamu ni jukumu lao kuutetea uongozi huo.
Chuki kati ya wananchi na Polisi inazidi, na inaendelea hadi kwa Wasanii walio upande wa CCM.
Tumeona hadi kwenye sherehe za harusi migawanyiko ya kiitikadi. Viongozi wa nchi wanachukiwak upita kiasi. Vifo vinashangiliwa kwa sababu aliekufa, japo ni Mtanzania, lakini hakuwa mwenzetu. Polisi wanaendelea kutumia fursa iliyopo kuendesha nchi.
Bado kidogo sana moto utalipuka tutaanza kupigana na kuuana wenyewe kwa wenyewe huku mitaani kwa visu na mawe na mapanga na marungu na fimbo.
Hivi viongozi wetu, na hasa Samia, hawaoni haya? Kama kweli ni viongozi wa wananchi na wazalendo wa kweli, na wanaona wazi wananchi wao wanaelekea kubaya, kwa nini wasichukue hatua kubwa kuondoa haya yote hata kama ni kutangaza serikali yote kujiuzulu ili tuanze upya?
Na nyie wanajeshi, hususa JWTZ, mmekaa tu kwa sababu Mkuu wenu alisharubuniwa? Hamuoni haya yanayoendelea? Mnafikia mahali mnaruhusiu askari wa nje kuingia nchini na silaha na kuua raia? Mnafikiri mlipewa jina la Jeshi la Wananchi kama utani?
Watanzania wenzangu, hasa nyie viongozi wa serikali, Samia na CCM yote, tufanye kitu kabla mambo hayajaharibika kabisa. Tuweke nchi mbele na vyama vyetu nyuma. Hali ni mbaya sana na inazidi kuwa mbaya hata zaidi.