Nchi Imeharibika, Laana Ipo juu ya Nchi, Busara Ikiendelea Kukosekana, Ndiyo Mwisho wa Tanzania ya Kale

Nchi Imeharibika, Laana Ipo juu ya Nchi, Busara Ikiendelea Kukosekana, Ndiyo Mwisho wa Tanzania ya Kale

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Yaliyotokea hii miaka ya karibuni, na hitimisho la October 29, ni uharibifu mkubwa wa Taifa, na uharibifu huu mkubwa umefanywa na watawala kwa kushirikisha vyombo vya ulinzi na usalama.

Miaka ya karibuni, mpaka hitimisho la October 29, vyombo vinavyoitwa vya ulinzi na usalama vimegeuzwa kuwa vyombo vya kuua na kuhatarisha usalama wa wananchi.

Fikiria hivi vyombo ndivyo vimekuwa vikihusika na kuteka watu wanaomkosoa mtawala!

Fikiria vyombo hivi vilitakiwa kuwa mfano wa maadili, vimegeuzwa kuwa vya wafilaji!

Fikiria vyombo hivi vilitakiwa kuwa walinzi wa wananchi, vimegeuzwa kuwa vyombo vya kigaidi, vya kutisha na kuwaua wananchi!

UKWELI HAUBADILIKI
Ukweli ni kwamba umwagaji damu unaofanywa na yule aliyetakiwa kutoa ulinzi, ni chukizo kuu mbele za Mungu, ni sawa na mzazi anayeamua kumwua mwanae. Mauaji ya namna hiyo huleta laana kuu.

Ni aheri vita ya baina ya taifa na taifa, ni aheri ya mauaji yatokanayo na vita kati ya taifa na taifa kuliko yale yanayofanywa na mtawala dhidi ya watu wake. Mauaji ya namna hiyo, hujenga chuki na uhasama wa kurithisha na usioisha. Uhasama huo husababisha mauaji ya muda mrefu ambayo hata yatakapotokea unaweza hata usijue chanzo chake. Aliye mtoto sasa, baba yake au kaka yake ameuawa, hana namna, amekaa kimya, miaka 10 baadaye ni mkubwa, anaoneshwa na majirani kuwa yule pale ni mtoto wa polisi aliyemwua baba yako, wapo watakaosema namwachia Mungu, wapo watakaosema kuwa lazima nilipe kisasi, unashangaa mtu ameuawa, sababu haijulikani, kumbe ni kisasi.

Kumbukeni yaliyomtokea karume, aliyemwua ni mtoto ambaye baba yake aliuawa na karume. Wakati baba yake anauawa, mtoto alikuwa shule, baada ya kumaliza shule alijiunga na jeshi, akafikia cheo cha luteni, kumbe dhamira yake ni kulipiza kisasi.

Hapa tulipofika, kwa damu za maelfu ya watu zilizomwaga, laana imemwagwa juu ya nchi. Nchi hii haitakuwa tena ni nchi ile tuliyoizoea. Na kwa kiburi na jeuri ya wale walioua wananchi, kamwe tusitegemee unafuu, bali hali kuzidi kuwa mbaya zaidi.

Mgojwa mahtuti huhitaji daktari bingwa wa uwezo wa pekee kuweza angalao kubadilisha uelekeo wa mgonjwa. Vivyo hivyo, nchi iliyo kwenye uelekeo mbaya kabisa, kama Tanzania, kwa sasa inahitaji kiongozi wa pekee kabisa aliyejaa hekima, ufahamu, upendo, dhamira njema, ambaye kwake madaraka si kitu kilicho muhimu kwake, bali muhimu ni uponyaji wa roho za watu zilizovunjika, na uokozi wa Taifa linaloelekea shimoni. Bahati mbaya kwa sasa hatuna kiongozi wa namna hiyo. Watawala hawa wanategemea bunduki za polisi, vifaru na ndege za jeshi watazidi kulitumbukiza taifa shimoni.

ukweli ni kwamba Chuki ikishaingia katika nchi, kamwe huwezi kuiondoa kwa mtutu wa bunduki wala kifaru cha jeshi, bali kwa hekima kuu inayopalilia mazungumzo, maelewano, kujishusha, kutenda haki isiyo na shaka wala walakini, na msamaha usio na mipaka.

Watawala hawa ambao kwao madaraka ni muhimu kuliko maisha ya binadamu, kamwe hawawezi kuliponya taifa lililoumizwa kwa damu za watu.

Tulikuwa tunayaona mataifa yale ambayo raia wake wanauana hovyo kama hawana akili, sasa Taifa letu limevunja record ya Dunia, ndani ya siku 3, mauaji ya watu zaidi ya 10,000. Hii ni wastani wa zaidi ya watu 3,000 kwa siku moja. Hakuna utawala uliowahi kuua watu wake kwa idadi kubwa namna hiyo kwa siku 1, isipokuwa Tanzania pekee. Tumeingia kwenye record ya Dunia kwa ubaya, baada ya kushindwa kulitambulisha taifa letu kwa mema!

Tuzidi kumwomba Mungu atuinulie watawala wenye hekima, awadondoshe watawala wauaji wenye kiburi, wanaoamini kwa wao kuwa viongozi wameondoka kwenye ubinadamu, na hivyo kuwa na mamlaka ya nani aishi na nani afe leo.
 
Ni kweli vijana tiktok wanajipanga sasa hivi ni hatari ee Mungu tusaidie
 
Back
Top Bottom