Uchaguzi 2020 Nchi imelipuka, kila kona, kila sehemu naona ni Tundu Lissu

Mwaka 2020 upo kivingine CCM lazima wakae
Eleza ni kipi kimefanyika ambacho ni katika mipango ya kuifanya ccm wakae? Kipi kilichobadilika katika yale mambo yenye kutumika na ccm kuendelea kubaki madarakani?

Kila mwaka upo kivingine ila kila mwaka wa uchaguzi ccm ndiye anayetangazwa mshindi,sasa mwaka huu kimefanyika nini kuzuia ccm asitangazwe mshindi?

Utaona hakuna kilichofanyika zaidi ya kujifariji na Lissu tu na kusahau 2015 kulikuwa na Ukawa kabisa ila haikufanikiwa.
 
Ni kweli kuwa CCM walifanya makosa sana kwa kutompeleka Magufuli kanda ya kusini; Jakaya, Majaliwa na Samia tu hawakuwa kete ya kutosha. Hiyo inaweza kuwa inawahakikishia CCM kukosa mikoa mitatu hasa kwa vile Nape ni mwana CCM ambaye yuko upande wa pili na haijulikani yeye anapiga kampeini za namna gani. Kwa hivyo Lindi, Mtwara na Ruvuma inaweza kuwa ni bye bye kwa CCM!!
 
Hii thread ni moja wapo ya vichekesho vinavyoendelea hapa JF.
 
Magufuli anafanya kazi kubwa wewe umekaa tu. Muda wote upo unabonyeza simu.
Angefanya kazi yake pasipo kututeka, kutupoteza, kututungia sheria kandamizi,... . ......... ingekuwa vyema. Lakini sasa....
 
Jiwe maji ya shingo Eti upinzani umekufa, wakina polepole na bashiru sio watu wazuri wamemtapeli Jiwe wa watu.
 
Endelea kujifurahisha na kuwadanganya wabeba mabox wa Ulaya na USA!
 
Kazi kubwa ipi? Kazi kubwa ni kuwabambikia kesi kesi za uonevu unyanyasaji wafanyabiashara wakubwa kwa kutumia TRA? Kazi kubwa ni kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani?
Huo wimbo ushachuja mitano tena kwa jpm
 

Mbona hapa jimboni Hai wanasema tofauti ? safari hii mambo ya mjini nawaachia wenyewe, mimi nitakuwa kijijini Lyamungo Sinde/ Machame mpaka tarehe 30/10 ngoja niongee ongee na Bi mkubwa kidogo hapa kijijini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…