sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,745
- 1,171
Toka kuasisiwa kwa kauli mbiu ya No reforms no election(NRNE) iliyopitishwa na kuazimiwa na mkutano mkuu wa CHADEMA huenda ikawa ndiyo operation iliyopokelewa kwa kishindo katika operations zote zilizowahi kupokelewa na jamii ya Watanzania.
Mapokeo yake yamejadiliwa kwa impact hasi/chanya lakini ikiendelea kuwa kwa kasi na kuzoeleka ndani ya masikio ya Watanzania.
Hakuna siku NRNE isitajwe ama kwa shari au kwa kheri!
✅Je ni kweli Taifa linahitaji Reforms!
✅Kwanini uchaguzi uwe sehemu ya
reforms!
✅Taifa bila reforms,zipi hasara zake
Hakuna shaka kabisa kwenye jambo hili ambalo Taifa linapitia. Tumechelewa kufanya mabadiliko ya kimfumo kwenye nchi yetu katika kipindi ambacho Dunia imefanya mabadiliko mengi yenye focus ya maendeleo ya Dunia na watu wake.
Bila reforms Taifa limetengenezewa ukiritimba mkubwa na kuhodhiwa kama mali binafsi ya kikundi fulani,Rais akiwa Mkurugenzi.
Kwa msingi huo Taifa linahitaji Reforms za kimfumo na kuliokoa kwenye mikono michafu ya wasaka tonge wenye kiu ya kujilimbikizia mali.
Nchi imepangaranyika kama mwanampotevu kwenye Biblia,imeacha misingi iliyokuwa nguzo za kushikilia haki,tumetengeneza pengi kubwa la Tajiri na Maskini kwa ratio ya 1:100,000 kitu ambacho ni hatari sana kwa mfumo mzima wa uongozi.
Rais ametengenezwa kuutumikia mfumo kinyume na takwa la katiba na kwa kuzingatia udhaifu huo wa katiba pia.
Katiba imebaki kuwa kijitabu cha kuapishia watawala na hugeuka lulu kwa watawala pale katiba inapotoa mwanya wa Kunyang'anya haki, mfano Rais kutoshitakiwa kwa makosa atakayo yafanya akiwa madarakani kwa mujibu wa ibara ya 46.-(1) & (2)
46.-(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii,haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Urais,ila tubkama angalau siku thelethini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani,Rais atapewa au atakuwa ametumiwa kwanza taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge,na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo,kiini cha madai yenyewe ,jina lake na anwaniya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa analodai.
Kwa mantiki hiyo ya katiba mfumo umemtengeneza Rais kuutumikia mfumo huo kama sehemu ya fadhila ya kuwekwa madarakani. Na kwa kuwa hakuna option ya kisheria ya kushughulikia Rais na kwa kuzingatia udhaifu wa kikatiba kujing'oa meno lazima Mtawala awe Dikitekta kulinda maslahi ya wachache dhidi ya wengi(umma),na hapo ndipo kuibuka kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unapotamalaki.
Reforms zinaelekezwa sana kwenye uchaguzi kwa kuwa ibara ya 8 ya Katiba ya JMT imetoa mwanya wa wananchi kuiweka serikali madarakani na kwa mamlaka hiyo serikali iliyopo madarakani imechukulia udhaifu wa Katiba kujitengenezea mifumo yenye kutoa fursa kwa watawala hao tu, umuhimu wa reforms kwenye uchaguzi wa kidemokrasia ni suala mtambuka sana.
Kimsingi moja ya eneo linalohitaji reforms kwa upana mkubwa na manusura ya kundi kubwa ambalo ni wahanga wa haki ni eneo la uchaguzi unaoiweka serikali madarakani,serikali iliyojiimarisha kuutumikia mfumo unaoiweka madarakani na kuifanya ibara ya 8 ya katiba kama format usoni mwa wapenda haki wa Dunia ndiyo pekee utakoweza ku maintain stability na discipline ya utawala bora.
Chama dola kilichoko madarakani kimekosa legitimacy ya kuwa chama cha siasa kwa kuacha misingi ya ustawi wa chama hicho kilichoachwa na waasisi wake.
CCM ina hofu ya kupoteza madaraka,lakini watawala wake wana hofu ya kupoteza walichokivuna kwa njia zisizo halali,hii inachagiza mfumo kuiruhusu CCM kuwa chama chinja chinja kwa gharama yeyote ili kuulinda mfumo huo,ambao sasa umeiba uchaguzi na kumiliki haki ya kikatiba pamoja na mapungufu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya wananchi kufanya maamuzi ya kuiweka serikali madarakani.
Wizi wa kura unaratibiwa na serikali,nasema hili kwa ushahidi wa macho yangu kupitia Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mjini kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa 2024,kuiba uchaguzi mbele ya wapiga kura takribani mitaa yote ya Jimbo zima la Kibaha Mjini chini ya OCD,DCO na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Aibu iliyofanyika inatulazimu kufanya mabadiliko ya sheria na kanuni zake zinazotungwa na Mkwe wa Rais ambaye wote hao ni wanufaika wa uchaguzi kwa maana ya wagombea.
Ili tuweze ku maintain peace and harmony kwa Taifa lazima mabadiliko ya kweli toka mwaka 1961 yafanyike sasa. Wapo wanaosema kwanini sasa na wapo wanashangaa kwanini serikali inayaogopa mabadiliko haya.
Mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi yanapaswa kwenda sanjari na mabadiliko makubwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977. Mchakato wake ulikwisha kamilika kilichokuwa kimebakia ni kura ya maoni.
Lakini kuna ongezeko la mambo mengi yanayoibuka sasa yanapaswa kuingizwa upya kwenye rasimu ya Warioba mbali na ile ya Samweli Sitta aliyoingiza kwa mlango wa nyuma.
Kipindi hiki ni muhimu sana kwa mabadiliko hayo ili kunusuru usawa na umoja wa Watanzania katika mgawanyo wa rasilimali za Taifa. Huenda mgawanyo wa mali za Muungano ni sawa, Zanzibar wanachukua chao kwa maslahi yao,je hawa Watanganyika mgawo wao unaishia wapi wakati ndiyo walipa kodi wakubwa kwa Taifa hili!
Tufikiri kwa kina kama kuna haraka ya kutiki October kama mnada wa rasilimali za Watanganyika au kufanya mabadiliko ya Katiba,sheria na Kanuni yatakayotoa haki za wananchi kuchagua serikali waitakayo itakayowajibika kwa wananchi kwa mujibu wa ibara ya 8.-(c).
Hivyo basi, Reforms ni muhimu sana kipindi hiki kwa kuwa mfumo umekuwa kichaka cha kulindia majambazi ya rasilimali.
Mungu bariki akili za Wahanga wa utawala ,Mungu angamiza fikra chafu dhidi ya wajumbe wa haki katika Mapambano ya Haki dhidi ya Batili