Nchi ipi ni Jirani mkubwa kwa Kenya?

Nchi ipi ni Jirani mkubwa kwa Kenya?

Carica_papaya

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2018
Posts
767
Reaction score
1,272
Kenya imezungukwa na nchi nyingi

1. Somalia
2. South Sudan
3. Uganda
4. Tanzania
5. Rwanda

Kati ya nchi hizo ni nchi gani ambayo Wakenya wapo na Ujirani + Undugu mkubwa nayo?
 
Ilikuwa Tanzania, Lakini kwa sasa nadhan nafasi hiyo imechukuliwa na Uganda
 
Uganda. Kuna sababu nyingi za Kenya na Uganda kuwa na muingiliano mzuri. Kuanzia historia ambapo Mabeberu kutoka Britain walitawala Kenya na Uganda kwa pamoja.

Uganda ikiwa protectorate ya kuzalisha chakula na Kenya ikiwa colony, yaani makaazi ya wazungu. Tuna makabila mengi ambayo yapo pande zote za border kama kabila la Teso na makabila mengine. Halafu kibiashara pia tunatangamana na Uganda kwa undani sana. 80% ya Ugandan imports inapitia Bandari ya Kenya.

Tuna reli iliyojengwa na beberu kutoka Mombasa hadi Kampala. Reli hii imefanya Kenya na Uganda zifanye biashara pamoja kuanzia enzi za ukoloni.

Halafu Uganda ni kati ya nchi tatu bora zinazonunua bidhaa za Kenya kwa wingi (Uganda is top three export destination for Kenyan products.).Halafu kuna repoti iliyotolewa juzi inayosema kuwa wakimbizi wengi wanaoishi Kenya wana uraia wa Uganda.
 
Ilikuwa Tanzania, Lakini kwa sasa nadhan nafasi hiyo imechukuliwa na Uganda
Hamna siku hata moja ambayo Tanzania imewahi kuizidi Uganda kwa urafiki wa karibu na Kenya. Maana urafiki wa Kenya na Uganda ulianza zamani wakati wa mabeberu. Tanzania pengine ni ya pili kwa umuhimu kwetu na hii inachangiwa sana na the fact that Kenya na Tanzania sote tunazungumza lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi ya taifa.
 
Aawapii Uganda waliowanyang'anya Migingo? Nadhani Somaliland ndo jirani Mkubwa wa Kenya!
Kwani kisiwa cha ekari moja tu ndicho kinachoweza kufanya urafiki kati ya Kenya na Uganda kuharibika? Halafu issue ya migingo ni ya juzi tu ilhali urafiki wa Kenya na Uganda ni wa zaidi ya miaka 120. Hususan urafiki wa kibiashara maana mabeberu walikuwa wanalima kahawa ndani ya nchi zote mbili na kuziexport kupitia bandari ya Mombasa
 
Kwa Tanzania tungekua na undugu ila sijui ni ujamaa au kitu gani maana hamuendani na yeyote, mpo tu wenyewe, licha ya nyie kumwaga damu nyingi kwa kile mliita kuikomboa Afrika lakini hakuna nchi moja mnayoendana nayo. Na kwa awamu hii ya tano ndio mlikalia kuti kavu kabisa maana mumeboronga kidiplomasia kote kote.

Nikirudi kwenye hoja, Waganda tunaendana nao vizuri sana, yaani Mkenya hata akienda Uganda hujihisi yuko nyumbani, ila Mkenya akisafiri kwenda Tanzania kwa shughuli yoyote inambidi kuvumilia sana akisubiri siku ya kugeuza, kuna wingu fulani hivi vigumu kueleza kulihusu lakini mtu huwa anahisi likimghubika.
 
Mimi naona ni Tanzania
.. Kwani wao wana Mzee wa vitendawili sisi tuna Mzee wa Ubwabwa Bahari mpaka Dodoma..
 
Hamna siku hata moja ambayo Tanzania imewahi kuizidi Uganda wa urafiki wa karibu na Kenya. Maana urafiki wa Kenya na Uganda ulianza zamani wakati wa mabeberu. Tanzania pengine ni ya pili kwa umuhimu kwetu na hii inachangiwa sana na the fact that Kenya na Tanzania sote tunazungumza lugha ya Kiswahili kama lugha rasmi ya taifa.
Huu ndiyo ukweli thabiti
 
Kwa Tanzania tungekua na undugu ila sijui ni ujamaa au kitu gani maana hamuendani na yeyote, mpo tu wenyewe, licha ya nyie kumwaga damu nyingi kwa kile mliita kuikomboa Afrika lakini hakuna nchi moja mnayoendana nayo. Na kwa awamu hii ya tano ndio mlikalia kuti kavu kabisa maana mumeboronga kidiplomasia kote kote.
Screenshot_2020-12-15 China-aided trans-Africa railway line likely to transform regional trade...png
 
Kenya imezungukwa na nchi nyingi
1. Somalia
2. South Sudan
3. Uganda
4. Tanzania
5. Rwanda
Kati ya nchi hizo Ni Nchi gani ambayo Wakenya wapo na Ujirani + Undugu mkubwa nayo
Kenya imepakana na Rwanda kivipi?

Kwa kifupi Kenya haina yeyote waliopo deep down loyal in friendship kati ya nchi zote wanazopakana, ni kisirani na kichomi kwa kila nchi jirani

Haiwezekani ugombane na kila jirani wewe tu.
 
Uganda. Kuna sababu nyingi za Kenya na Uganda kuwa na muingiliano mzuri. Kuanzia historia ambapo Mabeberu kutoka Britain walitawala Kenya na Uganda kwa pamoja. Uganda ikiwa protectorate ya kuzalisha chakula na Kenya ikiwa colony, yaani makaazi ya wazungu. Tuna makabila mengi ambayo yapo pande zote za border kama kabila la Teso na makabila mengine. Halafu kibiashara pia tunatangamana na Uganda kwa undani sana. 80% ya Ugandan imports inapitia Bandari ya Kenya. Tuna reli iliyojengwa na beberu kutoka Mombasa hadi Kampala. Reli hii imefanya Kenya na Uganda zifanye biashara pamoja kuanzia enzi za ukoloni. Halafu Uganda ni kati ya nchi tatu bora zinazonunua bidhaa za Kenya kwa wingi (Uganda is top three export destination for Kenyan products.).Halafu kuna repoti iliyotolewa juzi inayosema kuwa wakimbizi wengi wanaoishi Kenya wana uraia wa Uganda.
Kwa taarifa yako cargo ya Uganda imekuwa ikipitishwa 80% Kenya kuanzia 1980s ila kabla ya hapo tulikuwa tunagawana!
 
Kwa taarifa yako cargo ya Uganda imekuwa ikipitishwa 80% Kenya kuanzia 1980s ila kabla ya hapo tulikuwa tunagawana!
Sidhani kama tulikuwa tunagawana Cargo kabla ya 1950s maana sidhani kama transport corridor kati ya UG na TZ ilikuwa nzuri wakati ule. Pengine after Uganda kupata Uhuru wao 1962 ndio cargo ikaanza kupitishwa Tanzania. Lakini sina uhakika. Halafu nini ilifanya Uganda wapunguze kuimport cargo yao kupitia TZ?
 
Back
Top Bottom