Nchi isiyojali wanaomaliza masomo kwa alama za juu

Nchi isiyojali wanaomaliza masomo kwa alama za juu

Kuna sehemu nilikuwa,tukawainterview baadhi ya watu,mmoja alisoma Udom akiwa na 4.1......ila alikuwa hawezi hata kujieleza japo alikuwa na CV bora kuliko wote.......aliyeajiliwa alikuwa na 3.1 cos alikuwa very smart na alikuwa anajua anachokisema and well organised.......gipiei kubwa ni hatua bora ila baadhi yao nikukariri tu madesa......

Ila naunga mkono hoja,wenye GPA kubwa mzingatiwe
 
Inasikitisha Sana kwamba vijana wetu wanajitahidi kimasomo katika mazingira magumu Sana. Wakati mwingine fedha za mikopo ya kujikimu inachelewa, na hata wengine hawapati kabisa. Licha ya magumu yote hayo, unakuta kijana amejitahidi Hadi kufikia hatua ya juu ya ufaulu.

Wengine katika madaraja yanayofikia hadi GPA 4.2 na zaidi kwenye fani mbali mbali. Cha kushangaza ni kuwa serikali ambayo ndiye mwajiri na mlezi mkuu wa watu wake, Haina utaratibu wowote wa kuhakikisha hawa WALIOFANYA VIZURI wanaendelea na MASOMO ya juu zaidi kwa kuwapatia scholarship, au kuwaingiza katika programu inyowawezesha kujiendeleza zaidi. Hapa nawazungumzia vijana wanaohitimu Stashahada na Shahada ya kwanza.

Nchi yenye uwezo wa kununua midege kwa fedha taslimu, inashindwaje kuwawekea vijana wake utaratibu wa ajira au kuwandeleza kielimu wale WALIOFANYA VIZURI kwa viwango vya juu!? Tunawatelekeza bila kujali kwamba vijana hawa walikuwa wakikesha kuhakikisha wanapata ALAMA za juu wakiamini taifa lao litaziona juhudi zao.

Nimejaribu kuwasiliana na wakufunzi wa vyuo vikuu kadhaa ambao kwa masikitiko wamelalamika kuwa siku hizi wamefungwa mikono kwa kutoruhusiwa kuwachukua baadhi ya vijana wanaofanya vizuri ili wajiendeleze vyuoni kuja kujaza nafasi za kufundisha katika vyuo hivyo. Kwamba serikali haina mpango wa kujenga think tank ya Tanzania ni jambo la kusikitisha sana.

Ni wito wangu kwa wahusika, Mhe. Rais pamoja na wizara ya elimu ya juu, wizara ya utumishi, na tamisemi kukaa chini na kuliangalia jambo hili kwa jicho la pili.

"Mcheza kwao hutuzwa" ni msemo wa kiswahili wenye maana ya kuwazawadia mema wale wanaofanya mambo kwa uzuri. Sisi Tanzania tunajenga jamii ya aina gani ambayo hata yule anayefanya jitihada na kufanikiwa anakuwa hatambuliwi!

Serikali ifikirie kujenga watu zaidi kwa kuwajali hasa wale wanaofanya vizuri kwenye MASOMO. Haiwezekani vilaza na vipanga wote wawe "maji ga nyanza" eti kwa vile serikali inajali ndege na magorofa kuliko watu.

A concerned citizen.
Sasa unataka serikali iwafanyie nini?Wana GPA kubwa,na hawawezi kutengeneza chochote,mpaka wapewe ajira?!!Kama kweli akili zao Zinachaji sana,ilibidi wawe mstari wa mbele kutatua kelo za jamii,sasa wao walikuwa vipanga Darasani ,wakija kitaa,wanakuwa Kama kuku wa kisasa,hawawezi kuchukua chakula ,mpaka waletewe chskula!!!
Hao hawatufahi,
Miaka hiyo ya 60,vijana walijielewa,Kwanza kulikuwa hakuna hizi English medium,lakini tulipata vijana Kama Salim Ahmed Salim,huyu alikuwa balozi akiwa kijana wa form six tu,
Wa siku hizi,hata akiwa na PHD,ni mbulula tu,
 
G.P.A kwa sasa nimbwembwe tu naona,, mm nimemaliza chuo na 3.8 ila yote nimeipata kimaghumashi
 
MM SIJAFIKISHA GPA YA NNE + ILA MTOA MADA UTAPINGWA KWEL KWEL WATANZANIA WENGI WANA GPA CHINI YA NNE NA HAWATAKI KUSIKIA KUHUSU FEVA YOYOTE ILE KWA MTU YOYOTE MAALUM SO WANAHITAJ KILA KITU KIMWAGWE CHINI WATU WAGOMBEE

MAONI YANGU NI KWELI WANAOPATA GPA KUBWA WANATAKIWA KUENDELEZWA HATA KAMA KUNA BAADHI WANAZIPATA KIUJANJA UJANJA(KWENYE MSAFARA WA MAMBA NA KENGE WAMO) ILA SIO SABABU YA KUWANYIMA HAKI YAO WALIOFANA VIZURI CHUONI HATA KAMA KWA KUKARIRI(SIDHAN HATA HAO MAGENIUS WAKUBWA DUNIAN WASINGEKUWA WANAKARIRI WANGEWEZA KUWA NA MUENDELEZO WA KUFANYA MAMBO MAKUBWA)

HATA KATIKA MPIRA MFUNGAJI BORA HUTUNUKIWA ZAWAD BILA KUJALI KAZUNGUKWA NA NAN AU MAGOLI KAYAFUNGAJE YAAN GOLI NI GOLI TUU
Mkuu umenena iliyo kweli. Watanzania wengi tuna tatizo la ubinafsi na roho mbaya. Inawezekanaje wanafunzi wanaofanya vizuri wapatiwe nafasi toka msingi Hadi high school, Ila inapofikia degree au diploma, tudai kuwa wanakariri!!? Huku ni kuwatetea wapuuzi serikalini wasiotaka kutimiza wajibu stahiki kwa kuwa nao walipata GPA za vilaza. Inawezekanaje kiongozi wa nchi aamue kununua ndege kama njugu kwa kipato kidogo cha taifa, halafu tuone ni sawa kwa vijana wanaojitahidi kufanya vizuri kuachwa njia panda bila mwelekeo wowote. Tumekuwa kama nchi ya vichaa wasiojitambua!!!
 
Sasa unataka serikali iwafanyie nini?Wana GPA kubwa,na hawawezi kutengeneza chochote,mpaka wapewe ajira?!!Kama kweli akili zao Zinachaji sana,ilibidi wawe mstari wa mbele kutatua kelo za jamii,sasa wao walikuwa vipanga Darasani ,wakija kitaa,wanakuwa Kama kuku wa kisasa,hawawezi kuchukua chakula ,mpaka waletewe chskula!!!
Hao hawatufahi,
Miaka hiyo ya 60,vijana walijielewa,Kwanza kulikuwa hakuna hizi English medium,lakini tulipata vijana Kama Salim Ahmed Salim,huyu alikuwa balozi akiwa kijana wa form six tu,
Wa siku hizi,hata akiwa na PHD,ni mbulula tu,
Hujui kinachkojadiliwa, hivyo ni bora kukaa kimya. Mwalimu J. K. Nyerere alikuwa Ni kpanga darasani. Wakoloni hawakumuacha mtaani ajihangaikie ili kubuni mpango wa kujikomboa. Kwa kuwa alifanya vizuri, alipewa scholarship akaenda kusoma Edinburgh alikopata MA. Ni kosa kubwa kwa serikali kudhani kuwa kutengeneza think tank ya Taifa ni hasara. Maprofesa wengi ni wale waliotengenezwa na Mwalimu UDSM.
Mfano mwingine ni Rais Magufuli Ni zao la Chuo Cha Mkwawa kilichowekewa utaratibu Maalum ya kuzalisha walimu wa fani za sayansi. Hii ilikuwa Ni mwanzoni mwa miaka ya 80. Hata baada ya Mkwawa alipewa nafasi UDSM.
Leo waliopewa nafasi wanawalazimisha wengine wajitafutie nafasi!! Si haki hata kidogo. Kisha kwa hoja dhaifu kama hii yako inadai vijana ndiyo tatizo!! Si kweli, tuna uongozi usio na maono. Tunalipoteza taifa.
 
Sikujua kuwa hadi leo kuna Watu fulani wanaamini kuwa na GPA's za juu tena kutoka Local Varsities zetu ni Kipimo tosha cha Uwerevu wa Msomi.
Sasa kaka, kipimo Cha kufanya vizuri Chuo kikuu Ni kipi! Maana viwango vilivyopo Ni GPA. Kuna za chini, za Kati na za juu. Sasa hapa kwetu wale waliopata GPA za juu hawatambuliwi na serikali yetu kwa sasa. Binafsi naona hii si haki.
Sasa wapo ajinga wanaotaka hawa wasitambuliwe kama watu waliofanya jitihada. Si sawa hata kidogo. Kama Kuna mtu wa serikali humu na hasa wale wa TISS, Ni muhimu waliangalie suala hili, wasikalie tu kuisaidia CCM kuiba Kura na kupata madaraka wasiyojua namna ya kuyawianisha.
 
Back
Top Bottom