Nchi isiyojali wanaomaliza masomo kwa alama za juu

Kuna sehemu nilikuwa,tukawainterview baadhi ya watu,mmoja alisoma Udom akiwa na 4.1......ila alikuwa hawezi hata kujieleza japo alikuwa na CV bora kuliko wote.......aliyeajiliwa alikuwa na 3.1 cos alikuwa very smart na alikuwa anajua anachokisema and well organised.......gipiei kubwa ni hatua bora ila baadhi yao nikukariri tu madesa......

Ila naunga mkono hoja,wenye GPA kubwa mzingatiwe
 
Sasa unataka serikali iwafanyie nini?Wana GPA kubwa,na hawawezi kutengeneza chochote,mpaka wapewe ajira?!!Kama kweli akili zao Zinachaji sana,ilibidi wawe mstari wa mbele kutatua kelo za jamii,sasa wao walikuwa vipanga Darasani ,wakija kitaa,wanakuwa Kama kuku wa kisasa,hawawezi kuchukua chakula ,mpaka waletewe chskula!!!
Hao hawatufahi,
Miaka hiyo ya 60,vijana walijielewa,Kwanza kulikuwa hakuna hizi English medium,lakini tulipata vijana Kama Salim Ahmed Salim,huyu alikuwa balozi akiwa kijana wa form six tu,
Wa siku hizi,hata akiwa na PHD,ni mbulula tu,
 
G.P.A kwa sasa nimbwembwe tu naona,, mm nimemaliza chuo na 3.8 ila yote nimeipata kimaghumashi
 
Mkuu umenena iliyo kweli. Watanzania wengi tuna tatizo la ubinafsi na roho mbaya. Inawezekanaje wanafunzi wanaofanya vizuri wapatiwe nafasi toka msingi Hadi high school, Ila inapofikia degree au diploma, tudai kuwa wanakariri!!? Huku ni kuwatetea wapuuzi serikalini wasiotaka kutimiza wajibu stahiki kwa kuwa nao walipata GPA za vilaza. Inawezekanaje kiongozi wa nchi aamue kununua ndege kama njugu kwa kipato kidogo cha taifa, halafu tuone ni sawa kwa vijana wanaojitahidi kufanya vizuri kuachwa njia panda bila mwelekeo wowote. Tumekuwa kama nchi ya vichaa wasiojitambua!!!
 
Hujui kinachkojadiliwa, hivyo ni bora kukaa kimya. Mwalimu J. K. Nyerere alikuwa Ni kpanga darasani. Wakoloni hawakumuacha mtaani ajihangaikie ili kubuni mpango wa kujikomboa. Kwa kuwa alifanya vizuri, alipewa scholarship akaenda kusoma Edinburgh alikopata MA. Ni kosa kubwa kwa serikali kudhani kuwa kutengeneza think tank ya Taifa ni hasara. Maprofesa wengi ni wale waliotengenezwa na Mwalimu UDSM.
Mfano mwingine ni Rais Magufuli Ni zao la Chuo Cha Mkwawa kilichowekewa utaratibu Maalum ya kuzalisha walimu wa fani za sayansi. Hii ilikuwa Ni mwanzoni mwa miaka ya 80. Hata baada ya Mkwawa alipewa nafasi UDSM.
Leo waliopewa nafasi wanawalazimisha wengine wajitafutie nafasi!! Si haki hata kidogo. Kisha kwa hoja dhaifu kama hii yako inadai vijana ndiyo tatizo!! Si kweli, tuna uongozi usio na maono. Tunalipoteza taifa.
 
Sikujua kuwa hadi leo kuna Watu fulani wanaamini kuwa na GPA's za juu tena kutoka Local Varsities zetu ni Kipimo tosha cha Uwerevu wa Msomi.
Sasa kaka, kipimo Cha kufanya vizuri Chuo kikuu Ni kipi! Maana viwango vilivyopo Ni GPA. Kuna za chini, za Kati na za juu. Sasa hapa kwetu wale waliopata GPA za juu hawatambuliwi na serikali yetu kwa sasa. Binafsi naona hii si haki.
Sasa wapo ajinga wanaotaka hawa wasitambuliwe kama watu waliofanya jitihada. Si sawa hata kidogo. Kama Kuna mtu wa serikali humu na hasa wale wa TISS, Ni muhimu waliangalie suala hili, wasikalie tu kuisaidia CCM kuiba Kura na kupata madaraka wasiyojua namna ya kuyawianisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…