HERY HERNHO
Senior Member
- Mar 4, 2022
- 110
- 458
Poland na Hungary, ambazo ni nchi jirani na Ukraine, Jumamosi wiki iliyopita zilitangaza marufuku ya uagizaji kutoka Ukraine wa bidhaa za kilimo hadi Juni 30. Serikali za nchi hizo zinasema hatua hiyo inalenga kulinda wakulima wa ndani. Slovakia imefanya hivyo pia jana Jumatatu.
Bidhaa za kilimo za Ukraine zilikuwa zikisafirishwa hadi Afrika na maeneo mengine kupitia njia za baharini, lakini njia hizo hazikuweza kutumiwa kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Bidhaa za kilimo za Ukraine zimekuwa zikipitia Poland na nchi zingine wakati zikisafirishwa hadi kwenye bandari katika maeneo mengine ya Ulaya.
Lakini changamoto za usafirishaji, kama vile uhaba wa treni na malori ya mizigo, zimesababisha kiasi kikubwa cha bidhaa kukwama katika nchi hizo. Wakulima wa ndani wanahangaika kutokana na bidhaa za bei rahisi za Ukraine.
Ukraine inatoa wito kwa nchi hizo tatu kufikiria tena juu ya hatua hizo. Maafisa katika Wizara ya Kilimo na Chakula ya nchi hiyo wanasema, wakiwa wanaelewa taabu ya wakulima katika nchi hizo tatu jirani, wakulima wa Ukraine wapo katika hali mbaya hata zaidi