Naam sasa nchi zimeamuka, nchi mbali mbali duniani zinapeleka oda zao kupata chanjo ya CORONA. teyari jirani zetu Kenya chanjo hiyo imetua nchini mwao kwa GULF air majuzi.
Nchi zingine zimeenda mbali zaidi hazitoruhusu wageni kuingia nchini mwao pasi na kupata chanjo hiyo ya Corona
Pia shirika la afya duniani litatoa vitambulisho kwa wale watakao chanjwa ili wasitiliwe mashaka iwapo wataenda nchi nyingine.
Na vile vile kupata visa kuingia nchi nyingine siyo muda mrefu kuanzia sasa litakuwa ni sharti mhimu bila kuchanja no visa
Chanjo ni nini? Chanjo ni tone kidogo sana ambalo mtu hupewa aidha kwa kulamba au kupigwa sindano kwa madhumuni ya kuamsha uzalishaji wa askari wa kulinda mwili zidi ya ugonjwa huo huo, chanjo huwa ni vimelea vya ugonjwa huo huo unaochanjwa dhidi yake ila vimelea hivyo huwa vimepunguzwa nguvu sana kiasi haviwezi kuleta madhara zaidi tu ya kuamsha uzalishaji wa chembe chembe nwilini ambazo hupigana na vimelea vingine ambavyo vinasababisha ugonjwa husika.
Kwenye clinic za mama na mtoto hutolewa chanjo zinazofanana na Corona yaani chanjo zinazokinga magonjwa yanayosababishwa na virus mfano Surua. Hapa nchini watoto wamekuwa wanachanjwa zidi ya ugonjwa wa surua muda kidogo tangu tupate uhuru hadi sasa chanjo hiyo hutolewa clinic zote za mama na mtoto nchini, kwa hiyo suala hilo la chanjo siyo geni.
Pia kuna chanjo ya kichaa cha mbwa. Kichaa cha mbwa husababishwa na virus, mbwa huuguwa na kuweza kumuambukiza binadamu kwa kumng`ata. Ili binadamu asiuguwe huchanjwa chanjo zidi ya ugonjwa huo. Chanjo hiyo ni virus vya ugonjwa huo huo ambapo huwa vimepunguzwa nguvu kiasi haviwezi kuleta madhara hasi zaidi ya kuhamasisha uzalishashaji wa kinga mwilini endapo virus vingine vya ugonjwa huo vikiingia mwilini, na ikumbukwe kwamba kama mtu akiumwa na mbwa mwenye kichaa asipochanjwa akiuugua kifo huwa ni asilimia mia moja.
Kwa hiyo hata chanjo zidi ya ugonjwa wa Corona ni vimelea hivyo hivyo vya Corona ila vimepunguzwa nguvu sana kiasi haviwezi kuleta madhara ya mtu kuugua Corona bali kuhamasisha mwili kuzalisha chembe chembe nyingiii za kupigana na ugonjwa huo. Kwa hiyo mtu akichanjwa chanjo ya CORONA mwili huwekwa teyari endapo ataambukizwa virus vya Corona virus hivyo hupigwa kipigo kikali na chembe chembe kinga na virus huangamizwa haraka bila hata mhusika kujua kama ameambukizwa.
Nimeandika kwa kirefu kupinga wapotoshaji ambao eti wanadai wazungu wametengeneza chanjo ya Corona kwa nia ovu, siyo kweli ni kwa nia nzuri sanaaa. Mpotoshaji mmoja aliweka bandiko lake la upotoshaji MODS wakalitoa haraka sana ila mimi nilibahatika kulisoma na hii hapa ndiyo majibu yake.
Ingekuwa dunia hii tunaishi peke yetu sawa tungeweza tukapuuza chanjo kwa vile tunazitilia shaka ingawaje hatukutilia shaka kikombe cha babu au dawa za kujikinga na Corona toka Madagascar, sasa hatuishi peke yetu inatakiwa tuende sambamba na wenzetu vinginevyo watatutenga, sasa tukitengwa tutakuwa wageni wa nani?
Mungu huwa hajibu maombi bali hujibu jitihada za mtu aliyeomba, unafanya jitihada fulani halafu unaomba mungu abariki jitihada hizo ziweze kuleta mafanikio.
Aksanteni sana Mwenyezi Mungu awabariki.