Nchi masikini ili iendelee basi lazima;
Stage Ya Kwanza.
Kuzalisha mali ghafi ya kutosha mpaka kubakia (Hapa ni kilimo, uvuvi, ufugaji na uchimbaji).
Stage Ya Pili.
Uuzaji wa mali ghafi iliozidi (Haina matumizi) nje ya nchi/masoko ya nje ili kupata fedha za kufungua viwanda.
Stage Ya Tatu.
Kufungua viwanda vya kutosha kutengeneza mali ghafi zinazo zalishwa ndani ya nchi na kuwa bidhaa kutimiza uhitaji wa bidhaa kwa raia wake. Unapunguza uuzaji wa mali ghafi nje ya nchi/masoko ya nje na badala yake unapeleka bidhaa kuuza. Na kuongeza ajira kwa watu wake.
Stage Ya Nne.
Kuzalisha bidhaa zaidi ya mahitaji kwa raia wake, ili bidhaa zilizozidi kuweza kuuza kwenye masoko ya nje na kujipatia kipato.
Stage Ya Tano.
Uzalishaji wa mali ghafi na uzalishaji wa bidhaa viwandani kupita mahitaji ya raia.
NCHI HAIENDELEI KWA KUTEGEMEA KODI KABLA YA KUFIKIA STAGE YA 5. Huzalishi mali ghafi za kutosha na kubakia, huna viwanda vya kutosha kukidhi mahitaji ya bidhaa kwa raia. Halafu serikali itegemee kodi kuendelea au kudidimiza nchi isifikie malengo ya stage 5???